AMKA NA BWANA LEO 28/09/2021
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumanne, 28/09/2021.
*KAZA MWENDO KUIFIKILIA MEDE.*
*Nakaza Mwendo, niifikie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Wafilipi 3:14.*
▶️ Sisi sote tuna uzoefu tunaopaswa kuupata na misalaba ya kubeba. Ikiwa tutashughulikia raha zetu na kukidhi tamaa yetu na mapenzi, tutakutwa tumepungua katika siku ili ya kupatiliza na kutoa thawabu. Ikiwa tunaishi kwa kuwatendea wengine mema na kumtukuza Mungu, hatutajifikiria sisi wenyewe, bali tutajitahidi kuwa na faida ulimwenguni, kuwabariki wanadamu, nasi tutapokea Baraka ya "Vema" kutoka katika midomo ya Bwana.
▶️ Tunapaswa kuishi kwa ajili ya ulimwengu ujao. Ni huzuni sana kuishi maisha ya ovyo ovyo, yasiyo na malengo. Tunataka lengo maishani - kuishi kwa ajili ya kusudi fulani. Mungu atusaidie sote tuwe watu wa kujitolea mhanga, wenye kujijali kidogo, wenye kuisahau nafsi zaidi pamoja na masilahi ya kibinafsi; na kufanya mema, si kwa ajili ya heshima tunayotarajia kuipata hapa, bali kwa sababu hili ndio lengo la maisha yetu nalo litatoa jibu la hitimisho la kuwapo kwetu. Hebu maombi yetu na yapande kila siku kwa Mungu kwamba apate kutuvua ubinafsi....
▶️ Nimeona kwamba wale ambao wanaishi kwa kusudi, wakijitahidi kuwapa faida na kuwabariki wanadamu wenzao na kumheshimu na kumtukuza Mkombozi wao, ndio wale wenye furaha ya kweli duniani, wakati ambapo mtu ambaye hana utulivu, asiyeridhika, na anayetafuta hiki na kujaribu kile, akitumaini kupata furaha, daima analalamika kwa kuvunjwa moyo. Siku zote ni mhitaji, haridhiki kamwe, kwa sababu anaishi kwa ajili ya yeye mwenyewe basi. Hebu na liwe lengo lako kutenda mema, kutenda sehemu yako katika maisha kwa uaminifu.
▶️ *Kuna haraka na msisimko. Watu kwa pupa huwekeza mtaji wao wa pesa katika dhamana na hisa, wanakuwa matajiri kwa siku moja lakini bado hawaridhiki. Wanaendelea kuwekeza kwa matarajio ya wendawazimu. Hisa za benki zinashuka, aliyekuwa milionea asubuhi ni ombaomba usiku unapofika na njia ambayo wanafikiria kuwa ni bora kulimaliza jambo hili ni bastola, kamba au maji ya ghuba. Pesa ni Baraka wakati wale wanaozitumia wanakumbuka kuwa wao ni mawakili wa Bwana, kwamba wanasimamia mtaji wa Bwana, na lazima siku moja watoe hesabu kuhusu uwakili wao. Ni upendo wa pesa ambao Biblia inalaani kuwa ni shina la uovu wote - upendo ule ambao iwapo mtu atapoteza pesa maisha yale ya thamani kubwa aliyopewa na Mungu hufanywa si kitu kwa sababu pesa zimekwenda.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
Post a Comment