AMKA NA BWANA LEO 27/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

Jumatatu, Septemba 27, 2021

*USIPUUZE VITU VIDOGO VIDOGO*

_Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti._ Mathayo 6:27, 28

▶️ Niliitwa nipate kuzungumza (na hadhira kubwa huko Oakland, California) juu ya hitaji la kazi ya kina na kamilifu iliyo muhimu kwa kila nafsi, ili iweze kuimarishwa kwa nguvu zote, na jinsi inavyopasa kuwapo na juhudi za dhati kabisa ili kuwasaidia wote ambao tunahusianishwa nao, kwa maadili na mfano, kujitahidi kwa ajili ya kazi hii kamilifu inayopaswa kufanywa kwao kupitia kwa Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu.

▶️ Kuna uwezekano wa wengi kudanganyika kuhusiana na hali yao ya kiroho. Katika Kristo tutapata ushindi. Katika yeye tuna Mfano kamili. Wakati ambapo aliichukia dhambi kwa chuki kamili, aliweza kulia kwa ajili ya mwenye dhambi. Alikuwa na asili ya kiungu, huku akiwa na unyenyekevu wa mtoto mdogo. Alikuwa nacho katika tabia yake kile ambacho lazima tuwe nacho katika tabia zetu, uvumilivu usiochepuka katika njia ya wajibu, ambayo kutoka katika hiyo hakuna vizuizi au hatari zingeweza kumchepua, wakati moyo wake ulikuwa umejaa sana huruma kiasi kwamba ole za ubinadamu ziligusa moyo wake kwa huruma mno. Hakuweza kuwapita kando, kwa sababu Yeye ndiye aliyekuwa Mganga Mkuu wa kuponya maradhi ya jamii ya wanadamu.

▶️ Alikuwa ni Mkuu wa Mbinguni, akifanya kazi kwa ajili ya siku zijazo na bado akichukua na kurekebisha mambo kwa ajili ya wakati uliopo, bila kupuuza mambo madogo zaidi, lakini bado akifanya mipango mikubwa kabisa kwa ajili ya wakazi wa ulimwengu ulioanguka.

🔘 *Yesu, Mwokozi wa thamani kuu, alizungumza na wasikilizaji wake kuhusu wajibu wao wa kawaida katika maisha, utunzaji wao wa mavazi, na kula na kunywa kwao. Aliwafundisha kwamba mambo haya hayapaswi kuwa suala lenye mvuto wa kushughulisha, kana kwamba ni lazima waubebe mzigo huu siku zote. Aliwaelekeza kwa ndege na kuwaambia kwamba Baba yao wa Mbinguni anamjali hata shomoro mdogo. Yeye hutegemeza malimwengu, lakini bado anawajali ndege wadogo na ni kiasi gani zaidi atawajali wale ambao wameumbwa kwa mfano wake. Alielekeza kwa maua yenye uzuri unaong'aa, aliwaalika wayafikirie haya, na akatamka kuwa kwa usahili wao yaliushinda utukufu wa Sulemani; lakini bado huondolewa katika siku moja. Je! Ninyi si bora zaidi yao?*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments