AMKA NA BWANA LEO 15/09/2021
*KESHA LA ASUBUHI.*
*Jumatano, 15/09/2021.*
*KAMA YUDA ANGETUBU.*
"Aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake" *Yohana 13: 18.*
▶️ Ilikuwa ndani ya uwezo wa Kristo kujiokoa mwenyewe.
Alipozungumza maneno
( pale Gethsemane) " Mimi ndiye",Mara moja Malaika walimzunguka, na umati huo ulikuwa na ushahidi wote ambao wangeweza kuwa nao au ambao walipaswa kuwa nao kwamba Kristo alikuwa ndiye Uweza wa Mungu.
▶️Wakati Umati ule wa wauaji ulipofukuzwa na kwenda kwa kupepesuka, ukikamata hewa kama mhimili, na kuanguka chini kwa nguvu, lingekuwa ni jambo rahisi kwa Kristo kuwafanya wabaki kuwa wasiojiweza na kulala pale kifudifudi, nae angepita katikati yao bila kudhurika. Kwa Mwako wa kung'aa kwake na utukufu wake angeweza kuwafisha. Yuda alilitarajia hili, kwani mara nyingi Kristo aliwahi kuponyoka....
▶️ Si ajabu kwamba Yuda, hata wakati huo, bado alishikilia chuki yake na kusudi lake hadi mwisho.
Kama wakati ule angelitubu, kama angelikiri katika muda huu wa mwisho, ikiwa moyo wake wa msaliti ungelivunjika, angepokea msamaha. Lakini upinzani wa kishetani huongezeka katika Uwiano wa nuru iliyotolewa na kupingwa. Kusihi maonyo ya majanga na hatari kubwa zinazokuja, hazikubadilisha kusudi la Yuda,kwa sababu Moyo wake haukubadilika.
▶️ Mbele ya nuru na ushahidi alidhamiria kufuata mwelekeo wake Mwenyewe, na kufanya mapenzi yake mwenyewe. Ustahimilivu wa Kristo karipio lililotolewa kwa huruma likimjia hatimae kutoka katika midomo ya Kiungu, halikuvunja moyo wake mkaidi. Anaufanya moyo wake kuwa mgumu kwa upinzani wake wa muda mrefu. Anaona mahali ambapo nyayo zake zimeelekea,
Lakini mawakala wa kishetani wamemzunguka kila upande, naye hana uwezo wa kujiokoa kutoka katika mtego wao. Sifa za Ubinadamu zilizoshikiliwa kwa muda mrefu, kukataa kujisalimisha kwa nuru, sasa humfanya kipofu asiweze kuona matokeo yote.
*Yuda sio mtu pekee ambaye amepita kwenye Uwanja huu....*
*Yuda alikuwa mtu ambaye alikuwa na sifa za thamani.*
*Lakini hakuwa mtu wa kufundishika.* ...
▶️ Mtu anapokuwa na uhusiano na wale wanaobeba ujumbe kutoka Mbinguni, na akasikia lakini asiutende ukweli, Kwake ukweli huo unashushwa na kukosa kuwa na maana yoyote inayositahili kuzingatiwa.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Yuda.
▶️ Mwanadamu lazima auamini Ukweli; lazima abadilishe mwelekeo wake wa utendaji, akija kwenye upatanifu na nuru inayoangaza juu yake.
*MUNGU AKUBARIKI SANA.*
Post a Comment