AMKA NA BWANA LEO 13/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

Jumatatu, Septemba 13, 2021

*CHUNGA MANENO YAKO*

_Imeandikwa … tena imeandikwa … Kwa maana imeandikwa._ Mathayo 4:4-10

📖 Wengine ambao katika nyakati zilizopita waliheshimiwa na Mungu, wamenaswa na udanganyifu wa adui. Wameonywa juu ya hatari yao, lakini kwa kukataa kusikia maonyo yaliyotumwa kwao, wamedanganyika zaidi na zaidi, hadi hatimaye wanakutwa wakipambana dhidi ya Bwana na dhidi ya wafanyakazi wake. 
 
📖 Wale ambao wanasimama juu ya mwamba wa ukweli wa milele wakati mwingine watakutana na upinzani ambao utahitaji vitendo thabiti zaidi. Kwa nyakati kama hizo hebu kila neno lipimwe kwa uangalifu, usije ukajeruhi roho za wale unaotaka kuwasaidia. Zuia ulimi wako kama kwa hatamu. Kumbuka kwamba Mungu hajakupa kazi ya kuwahukumu ndugu zako…
 
📖 Kutoka katika Neno la Mungu kukusanya faraja yote na kutiwa moyo kote kunako wezekana, na uwasilishe hivi kwa roho zinazopambana na mifadhaiko na shida. Lakini kamwe usilete lawama za kukosoa dhidi ya wale ambao wamedanganywa… 
 
📖 Katika kukutana na adui jangwani, jibu la Kristo kwa mawazo yake maovu lilikuwa, “Imeandikwa” wakati Shetani alithubutu kudai umiliki wa ulimwengu wote, na kumwambia Kristo amwabudu kama Mungu, yeye ambaye kwa neno moja angeliita kuwa msaada wake majeshi ya malaika, alisema tu, “ Nenda zako, Shetani, kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake” (Mathayo4:10). Ukali wa pambano hili sisi tunaujua kwa sehemu tu. Ilionekana kana kwamba Mwokozi angekufa kwenye uwanja wa vita, lakini Alimhimili yule adui mwerevu. Maneno yake yaliyochaguliwa kwa uangalifu sana, yalikuwa makali kama upanga ukatao kuwili. Shetani alishindwa kabisa. Aligundua kuwa Mkuu wa Uzima asingeliweza kudanganywa kwa hila yoyote ile.
📖 Sasa tuko katika uwanja wa mapambano….
 
📖 Hebu Neno la Mungu na liwe somo letu….
 
🔘 *Kwa wote wanaomwamini, Kristo huwapa nguvu ya kufanyika wana wa Mungu. Wale ambao kwa jinsi hiyo wameitwa kuwa ni washiriki wa familia ya kifalme wataishi kwa ajili yake yeye ambaye ni upatanisho wa dhambi zao. Kadiri wanavyofuatilia ili kujua ukweli, miguu yao inasimikwa kwenye msingi wa imara. Si mafuriko wala dhoruba itaweza kuuzoa msingi wao.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments