AMKA NA BWANA LEO 12


*KESHA LA ASUBUHI*

Jumapili, Septemba 12, 2021

*WAKRISTO KWA SASA*

_Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake; ili atakapotokea, tuwe na ujasiri, wala tusione haya mbele yake wakati wa kuja kwake._ 1 Yohana 2:28

📚 Wengi wanaelekea kuwa Wakristo wakati mwingine, lakini bado hawataki kuanza… si tu kwamba ninyi wenyewe mnapoteza mengi kwa kumpa adui sehemu bora zaidi ya maisha yenu, lakini mnawalea watoto wenu katika kupooza mambo ya milele. Wana mfano wenu, wote katika upande usio sahihi. Kupuuza kwenu kunawanyima maarifa yale ambayo Mungu hufanya iwe ni wajibu wenu kuwapa ili wapate kujifunza kupenda, kuwa na kicho, na kutii matakwa ya Mungu…
 
📚 Watoto wenu ni hodari na wepesi kutambua wawapo mbele ya watu wazima. Mnatengeneza akili zao kufikiri kama mnavyofikiri, kutenda kama mnavyotenda; wala si kupiga magoti kwa Mkuu wa ulimwengu kwa sababu hamfanyi hivyo. Ni vibaya sana na ya kutisha kutafakari juu ya upotevu wa nafsi zenu isipokuwa mmejisalimisha kwa Mungu, kufikiria kwamba ninyi wenyewe hamwingii katika mlango wa wokovu, lakini ni vibaya zaidi kufikiri ya kwamba mnazuia njia ya kuingia kwa watoto wenu…. Sahau mara moja yote kuhusu hadhi yako na nafasi yako kijamii, na anza mbele ya watoto wenu kama wanafunzi katika shule ya Kristo. Waambie ukweli kwamba umekosea kwa kupuuza kukiri wewe mwenyewe kuwa mtoto wa Mungu. Waambie kuwa unataka kwamba kama familia sasa mnapaswa kuanza kuishi kwa ajili ya Mungu, na kisha soma na kuomba pamoja na watoto wako…. 
 
📚 Unaweza kupata pumziko na amani pale tu unapoipata kwa Yesu.. ulimwengu, kanuni zake na desturi zake, ni wazazi wa mateso yasiyo na idadi. Wengi wanateseka kwa matamanio ambayo hayajakidhiwa. Wanajibebesha mizigo – tamaa zao ambazo hazijakidhiwa. Pamoja na hukumu ya dhamiri – kutokupatana na Mungu, na kwa kuhofia chuki yake na ghadhabu – kuishi kwao ni jambo la wasiwasi endelevu. Kuna ukosefu wa faraja ya Mbinguni katika mateso. Wanaogopa adhabu. Kuna ubashiri wa kuogofya wa siku za mbele. 
 
📚 Fidia imetolewa kwa ajili ya roho, kafara kubwa sana – mfalme kuwafia raia waasi, ili wapate kuokoka kutoka katika dhambi, upotovu, na taabu. Wote wanaweza kupata msamaha, utakaso, na Mbingu kupitia kujishusha sana kwa Mwana wa Mungu…..
 
🔘 *Njoo wakati ambapo sauti tamu ya Rehema inakuita.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

DOWNLOAD APPLICATION YETU PLAY STORE SASA, KUTUMIA NI BUREE👉📱

No comments