AMKA NA BWANA LEO 10/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

Ijumaa, Septemba 10, 2021

*KRISTO HAJAGAWANYIKA*

_Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka …. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe, wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi._ 1 Wakorintho 12: 18-21

✍🏻 Kwa sababu watu hawana chapa ile ile ya tabia, hii sio sababu ya kuwafanya watengane. Ikiwa sisi ni watoto wa Mfalme wa Mbinguni, hatutahitilafiana kiasi kila mmoja kusimama katika njia ya mwingine. 
 
✍🏻 Ni kwa amri ya Bwana kwamba watumishi wake wana karama mbalimbali. Ni kwa kupanga kwake watu wenye mawazo tofauti huletwa kanisani, kuwa watendakazi pamoja naye. Kuna akili nyingi mbalimbali tutakazokutana nazo, na karama mbalimbali zinahitajika. Watumishi wa Mungu wanapaswa kufanya kazi kwa upatanifu-amani kamili. Ninamshukuru Bwana kwa kuwa sisi sote hatufanani kabisa, wakati ambapo sisi sote tunapaswa kuwa na roho moja –roho iliyokuwa ndani ya Kristo. Mtume Yohana hakuwa sawa na mtume Petro. Kila mmoja alitakiwa kutiisha sifa yake bainishi na kulainisha tabia, ili wapate kusaidiana, kupitia kwa imani na utakaso wa ukweli. 
 
✍🏻 Ni haki ya Kristo ndio inayotutangulia. Ni tabia yake ndiyo tunapaswa kuiiga. Halafu nini? – Utukufu wa Bwana utakuwa nyuma yetu. Kiongozi wetu ametangulia mbele yetu, na tunapomfuata Yeye hutupatia haki yake, ambayo inadhihirishwa katika maisha yetu kwa maisha yaliyopangiliwa vizuri na mazungumzo ya kumcha Mungu. Ni imani ya matendo ndio vinatufanya sisi kuwa Wakristo, vikituandaa kukaa pamoja katika makao ya Mbinguni pamoja na Kristo. 
 
✍🏻 Je Kristo amegawanyika? – Hapana. Kristo anayekaa rohoni hatagombana na Kristo aliye katika roho nyingine. Lazima tujifunze kuvumilia sifa bainishi za wale wanaotuzunguka. Ikiwa mapenzi yetu yapo chini ya mapenzi ya Kristo, tunawezaje kuhitilafiana na ndugu zetu? Ikiwa tunahitilafiana, tunaweza kujua kwamba ni kwa sababu nafsi inahitajika kusulubiwa. Yeye ambaye Kristo anamfanya kuwa huru yuko huru kweli kweli. Hatuko kamili katika Kristo isipokuwa tunapendana kila mtu na mwenzake kama vile Kristo alivyotupenda. Tunapolifanya hili, kama Kristo alivyotuamuru, tutatoa ushahidi kwamba tumekamilika ndani yake. 
 
🔘 *Ni lazima tuwe na imani ile ambayo manabii waliitabiri na mitume waliihubiri – imani inayotenda kazi kwa upendo na kuitakasa roho.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments