AMKA NA BWANA LEO 07/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumanne, 07/09/2021.

*KIBURI HUTANGULIA ANGUKO.*

*Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.*
1 Wakorintho 10:12

▶️ Mara tu kabla ya anguko la Petro. Kristo alimwambia, “Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano” (Luka 22:31).
 
▶️ Urafiki wa Mwokozi kwa Petro ulikuwa wa kweli kiasi gani! Onyo lake la huruma kiasi gani! Lakini onyo hilo lilichukiwa. Katika kujitosheleza Petro alitangaza kwa ujasiri kwamba kamwe hatafanya kile ambacho Kristo alikuwa amemwonya. “Bwana,” alisema, “mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.” (aya ya 33). Kujiamini kwake kulithibitisha uharibifu wake. Alimjaribu Shetani apate kumjaribu akaanguka kutokana na ujanja wa adui mwerevu. Wakati ule ambapo Kristo alikuwa akimhitaji kupita nyakati zingine zote, alisimama upande wa adui, na akamkana Bwana wake waziwazi….
 
▶️ Wengi leo husimama pale Petro aliposimama, ambapo kwa kujiamini alitangaza kwamba asingemkana Bwana wake. Na kwa sababu ya kujitosheleza kwao, wanakuwa mawindo rahisi kwa hila za Shetani. Wale wanaotambua udhaifu wao huamini nguvu iliyo juu kuliko nafsi. Na pale wanapomtazama Mungu, Shetani hana nguvu dhidi yao. Lakini wale wanaojiamini hushindwa kwa urahisi. Hebu na tukumbuke kwamba ikiwa hatutii maonyo ambayo Mungu anatupatia, anguko liko mbele yetu. Kristo hatazuia majeraha kwa yule anayejiweka mwenyewe bila kualikwa kwenye eneo la adui. Anamruhusu yule anayejitosheleza ambaye anatenda kana kwamba anajua zaidi ya Bwana wake, asonge mbele kwa nguvu yake ya kudhaniwa. Ndipo huja mateso na maisha yaliyoharibika, au huenda kushindwa na kifo. 
 
▶️ Katika vita, adui hutumia sehemu zenye ulinzi dhaifu kwa wale anaowashambuli. Hapo anafanya mashambulizi yake makali kabisa. Mkristo hapaswi kuwa na sehemu zenye udhaifu katika ulinzi wake. Inabidi awekewe vizuizi na msaada ambao Maandiko yanampa yule anayefanya mapenzi ya Mungu. Nafsi iliyojaribiwa itachukua ushindi, ikiwa itafuata mfano wa yule aliyemkabili mjaribu na neno, “Imeandikwa.” Anaweza kusimama kwa usalama katika ulinzi wa “asema Bwana”….
 
▶️ *Bwana anaruhusu watoto wake kuanguka; na kisha, iwapo watatubu makosa yao. Yeye huwasaidia kusimama juu ya uwanja mzuri. Kama moto unavyosafisha dhahabu, vivyo hivyo Kristo huwatakasa watu wake kwa majaribu na majaribio.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

FOLLOW US @Binagotv👇🏾
Pia download Application yetu PLAY STORE👉📱 kama bado, ingia play store andika BINAGO TV Halafu download ⬇🔄

No comments