AMKA NA BWANA LEO 02/08/2021
*KESHA LA ASUBUHI*
*Alhamisi Septemba 2,2021*
*IMEANDIKWA KUWA ONYO KWETU*
" _Atawaongoza wanyenyekevu katika hukumu, Naye atawafundisha wanyenyekevu njia yake._ "
Zaburi 25:9
▶️ Mungu atafanya kazi na wale ambao wataisikiliza sauti Yake.Neno la Mungu linapaswa kuwa ndiye mshauri wetu, na linapaswa kuongoza uzoefu wetu.
Masomo ya historia ya Agano la Kale, kama yatachunguzwa kwa uaminifu, yatatufundisha jinsi ambavyo hili linaweza kuwa. Kristo,aliyefunikwa na nguzo ya wingu wakati wa mchana na nguzo ya moto wakati wa usiku, alikuwa ndiye kiongozi na nuru ya wana wa Israel katika kutangatanga kwao jangwani. Hapa alikuwapo kiongozi asiyeweza kukosea.
▶️ Katika uzoefu wao wote mbalimbali,Mungu alikuwa akijaribu kuwafundisha utii kwa Kiongozi wao wa Mbinguni, na imani katika nguvu Yake ya Kuwakomboa. Kukombolewa kwao kutoka katika mateso huko Misri, na kupita kwao Bahari ya Shamu,Kuliwadhihirishia uweza wake wa kuokoa. Walipoasi dhidi yake, na kwenda kinyume na mapenzi yake, Mungu aliwaadhibu.
▶️Walipodumu katika Uasi wao, na kudhamiria kufanya walivyoona wao wenyewe, Mungu aliwapa kile walichokiomba, na kwa njia hii aliwaonesha kwamba,kile alichowazuilia, Alikizuia kwa faida yao wenyewe. Kila hukumu iliyokuja kama matokeo ya manung'uniko yao ilikuwa ni fundisho kwa Umati ule mkubwa, kwamba huzuni na mateso kila wakati ni matokeo ya kukiuka sheria za Mungu.
▶️ Historia ya Agano la Kale ilirekodiwa kwa faida ya wale ambao wataishi katika vizazi vya baadaye. Masomo ya Agano Jipya pia yanahitajika sana.
Hapa tena Kristo ndie Mwalimu akiwaongoza watu wake wajitahidi kupata hekima ile itokayo juu,na kupata elimu ile katika haki ambayo itatengeneza tabia katika mfano wa kiungu.
▶️ *Maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya yanafundisha kanuni za utii kwa amri za Mungu kama masharti ya kupata maisha yale ambayo yanalingana na maisha ya Mungu, kwa kuwa ni kwa utii ndipo tunakuwa washirika wa tabia ya Uungu, na kujifunza kuokolewa kutoka katika uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.*
▶️ Kwa hiyo maneno yake ya hekima yanapaswa kuchunguzwa, amri zake kutiiwa, kanuni zake, ambazo ni za thamani sana kuliko dhahabu, kutumika katika maisha ya kila siku.
Post a Comment