AMFUMUA NYUZI BAADA YA KUMSHONA KISA KUKOSA GHARAMA
Wizara ya Afya Nchini imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii inayozunguka mitandaoni kuwa, mtaalamu wa Afya katika kituo ambacho bado hakijatambuliwa amemshona mgonjwa jeraha kisha akalifumua kwa madai kuwa mgonjwa huyo hakuweza kulipia gharama.
Ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu.
Hivyo, wizara inaomba wenye taarifa za wapi huku au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya wizara ya afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya waziri wa Afya ya 0734124191.
Hata hivyo, Ofisi ya Rais TAMISEMI imesema Tukio hili lilitokea Mwezi Julai, 2021 na mtumishi aliyekiuka miiko ya Udaktari anaitwa Jackson Meli ni Clinical Officer wa Kituo cha Afya Kerenge Tarafa ya Magoma, Halmashauri ya Wilaya ya korogwe Mkoani Tanga.
"----->Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa Hati ya Mashtaka na pia ameshafikishwa kwenye Baraza la Taaluma ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda Kinyume na Miiko ya Taaluma ya Udakrari."---- TAMISEMI
Usisahau Ku-Subscribe Youtube Channel Ya BINAGO TV KWA HABARI ZAIDI,. KWA KUBONYEZA ALAMA YA KENGERE 👉🔔.
Post a Comment