Ofisi ya Rais - TAMISEMI imetangaza kusikitishwa na kitendo cha watumishi wawili (2) Mwl. Omary Abdallahemed Kwesiga Mkuu wa Idara Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Scolastica L. Kanje Afisa Muuguzi Msaidizi hospitali ya Mkoa wa Arusha kufanya igizo kwenye zoezi la chanjo ya COVID-19 kinyume cha Taratibu na kanuni za Utoaji wa Chanjo hivyo kuleta sitofahamu kwa wananchi kuhusu zoezi la Chanjo linaloendelea nchini kote.
Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI kumsimamisha kazi Mwl. Omary Abdallahemed Kwesiga Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Aidha, ameagiza Scolastica L. Kanje Afisa Muuguzi Msaidizi apelekwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga kwa hatua zaidi.
0 Comments