Advertisement

Responsive Advertisement

CLATOUS CHAMA ALETA GUMZO INSTAGRAM, MO DEWJI AKASIRIKA

Leo kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kiungo wa
Simba Clatous Chama akiwa Live Insta aliulizwa
swali kuhusu kuondoka kwa Haji Manara ndani ya
klabu ya Simba, kwenye kujibu Chama alimsifia Haji kitendo ambacho kilimkera mwekezaji wa klabu ya Simba Mohamed Dewji "Mo".

Mo alimuuliza Chama "Haji ndiye aliyekulipia ada ya uhamisho ?" Chama akiwa anamjibu Mo alijibu kwa kuomba msamaha kama amemkwaza, Mo
akamuuliza tena Nani aliyekulipa Ada Haji? baadae Chama alipotaka kujibu Mo akamwambia anatoka kwenye mkutano huo wa Insta.

NOTE. na Mchambuzi wa Michezo Yossima Sita JR.✍

1.Kumekuwa na kampeni ya wachezaji wa klabu ya Simba kuwa upande wa Mo kuhusu press ya Haji na Tetesi za Mohamed kuwaambia watu wake wa karibu anataka kuondoka Simba.

2. Pia asubuhi Haji Manara alipost kwenye akaunti
yake akidai kuwa Mohamed Dewji 'Mo' amewalipa
wachezaji wa Simba na kuwataka waongelee juu ya Press ya Haji na kumuunga mkono yeye.

3. Nilikuwa na wasiwasi na kauli ya Haji Ila alichofanya Mo kwa Chama nimeanza kuamini hiki kitu hii tabia ni mbaya kwa mwekezaji kujiona yeye ndio kila kitu na kuwataka wachezaji kuwachagulia marafiki.

4. Nilikuwa na wasiwasi na kauli ya Haji Ila alichofanya Mo kwa Chama nimeanza kuamini hiki kitu hii tabia ni mbaya kwa mwekezaji kujiona yeye ndio kila kitu na kuwataka wachezaji kuwachagulia marafiki.

5. Pia wana Simba wanatakiwa kujua Mo ni
muwekezaji na sio mfadhili ndani ya Simba
kuwataka wachezaji wamuunge mkono si jambo
njema kazi ya mchezaji ni kucheza mpira na si
vinginevyo kuwaaingiza wachezaji kwenye ugomvi
wao wa management ni kuwakosea heshima.

Post a Comment

0 Comments