WANAFUNZI WATATU WAVAMIWA NA KUSHAMBULIWA NA SIMBA

Kamanda mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema tarehe 03.08.2021 muda wa 22:00hrs huko maeneo ya kijiji cha Ngoile wilaya ya Ngorongoro na Mkoa wa Arusha kulitokea tukio la kuuawa watoto watatu na simba wanafunzi wa shule ya Msingi Ngoile ambao ni OLOBIKO S/O METUI, miaka 10, NDASKOI S/O SANGAU, SYRS, SANKA S/O SANING'O 10YRS, wote ni wanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Ngoile ambao walifariki dunia baada ya kushambuliwa na Simba pia mtoto mwingine aitwaye KIAMBWA S/O LEKTONYI 11YRS alijeruhiwa na kundi hilo la simba ambao jumla
yao ni watoto wanne wote wanafunzi wa shule ya msingi Ngoile.

"----->Chanzo cha tukio hilo ni baada ya wanafunzi hao kutoka shule ambapo walifika majumbani mwao na walikwenda kutafuta mifugo yao iliyokuwa imepotea porini kitendo kilichopelekea kushambuliwa na wanyama hao wakali aina simba"---- MASEJO

Aidha, amesema majeruhi amelazwa katika Zahanati ya Kata ya Olbalbal kwa matibabu zaidi pia, ambapo pia miili ya marehemu wote imefanyiwa uchunguzi wakidaktari na ndugu warehemu wamekabidhiwa miili hiyo.

"----->Nitoe wito kwa jamii za kifugaji kuchukua tahadhari kwa watoto wadogo pindi wanapowapa majukumu ya uangalizi (kuchunga) mifugo hususani katika vijiji vinavyopakana na hifadhi ili kuepusha madhara makubwa."---- MASEJO

No comments