WAHAMIAJI 9 WA BURUNDI WATIWA MBARONI MKOANI SHINYANGA
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Naibu Kamishna (DCI) Rashid Magetta amethibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao ikiwa ni matokeo ya oparesheni inayoendelea Mkoani humo dhidi ya wahamiaji haramu.
Jumla ya raia 9 wa Burundi wamekamatwa Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wakiwa wamepangiwa nyumba na mtanzania ambaye alikuwa anawatumikisha ktk kazi za vibarua hususani kuchunga ng'ombe na kuandaa mashamba ya tumbaku.
Pamoja na Warundi hao mwenyeji wao raia wa Tanzania na ndugu zake wawili pia wamekamatwa na kesho wote watafikishwa mahakamani, kujibu mashtaka ya kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria sambamba na makosa ya raia wa Tanzania kuhifadhi na kuwatumikisha wahamiaji hao.
DCI Magetta amewataka wananchi mkoani humo kuacha kabisa vitendo vya kusafirisha na kuhifadhi wahamiaji haramu kwani vitendo hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria ya Uhamiaji sura 54 Rejeo la mwaka 2016 pamoja na kanuni zake ambapo watuhumiwa wakithibitika kutenda makosa hayo adhabu yake ni kifungo cha miaka ishirini (20) au kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini (20) au vyote kwa pamoja.

Post a Comment