Advertisement

Responsive Advertisement

SERIKALI YAENDELEA KUWAJALI WAKULIMA WA KOROSHO

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husseina Bashe amesema wanaendelea kuwahudumia wakulima wa korosho hasa ukizingatia zao hilo ndo linaongoza Kwa Mauzo ya Nje.

"Kwa kipindi cha miaka 3 zao hili lilikabiliwa na changamoto mbali mbali na kupeleka uzalishaji kushuka toka Tani 320,000 mpaka 205,000.
Pamoja na changamoto za kisera (ambazo Serekali imezifanyia kazi), Tulibaini tatizo kubwa ni uwezo wa wawakulima kuhudumia zao lenyewe"

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mh Rais Samia Suluhu Hassan (SSH) iliamua kutoa Ruzuku ya pembejeo Kwa wakulima wa korosho, tunatarajia Kugawa Tani 21,000 za Sulphur na Lita 1,200,000 (1.2m) za Dawa za Maji"

"Mpaka sasa Tumegawa Jumla ya Tani 11,823 za Sulphur na Lita 725,859 za Maji, na jana ilikua siku nzuri ambapo tumepokea shehena ya Lita 130,000 za Dawa za maji"

"Kwa niaba ya wizara ya kilimo na wakulima naishukuru TPA kwa wiki hizi 2 tumepokea Jumla ya meli 4 ambazo zimebeba Viwatilifu na Leo tumepakua meli ya mwisho.

Usambazaji huu utakua ni mkubwa Kwa Idadi ya viwatilifu kusambazwa katika Historia ya zao la korosho.Mwaka 2017/18 Sulphur ilotumika ilikua Tani 8,000 na Dawa za maji zilizotumika ni Lita 350,000 na kutupatia uzalishaji wa Tani 320,000 za korosho"

"Matumizi ya Dawa za maji yatakua makubwa kuliko Sulphur na huu ni ushauri wa NALIENDELE
Nawashukuru sana wakulima wa Korosho wengi wamefufua mashamba yao na kuongeza Mahitaji ya pembejeo"

"Kwa msimu ujao tutahakikisha Inshaallah pembejeo kufika nchini kabla ya mwezi Machi,
Na nikumbushe Kinachotolewa na serekali ni Ruzuku, wakulima nao wanawajibu kuendelea kujihudumia vile vile, ninawakumbusha ndugu zangu wakulima kauli isemayo “Ukibebwa Jishike"

"Thamani ya Ruzuku hii ambayo italipiwa kwa Mfumo wa PPP ni wastani wa 61bn tukio hili la kihistoria ni dhamira ya Mh Rais SSH kuwekeza kwenye Sekta ya kilimo"

"Majaribio haya ya Korosho na Pamba tutayapima matokeo yake na kujenga mfumo wa Input Financing kwakutumia Zao lenyewe kujiendesha kwenye Mazao Mengine"

"Nawashukuru sana Wakulima wa korosho kwa Uvumilivu na kushirikiana katika kukabiliana na changamoto zote ktk kipindi hiki cha marebisho (Reforms)"---- HUSEEIN BASHE


Post a Comment

0 Comments