Advertisement

Responsive Advertisement

WATU KUANZA KUNUNUA MAHINDI KILO MOJA KWA TSH. 500/=

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema serikali ya mama Samia baada ya kufanya Tathmini na kuona bei ya Mahindi imeshuka katika Mikoa ya Rukwa , Katavi, Mbeya, Njombe na Ruvuma imeamua kutoa bei ambayo itamlinda mkulima ya Tsh 500 Kwa kilo.

"Kuanzia tarege 15 Agosti 2021 NFRA wataanza kununua Mahindi katika Mikoa hiyo"

"Maamuzi haya ni katika Jitihada za kumlinda Mkulima kutokana na Ongezeko la Uzalishaji mazao na bei ya mavuno kushuka mpaka Tsh 200 kwa kilo katika maeneo hayo, hasa ukizingatia Mbolea imepanda DUNIANI, tumeona njia ya kukabiliana na changamoto hii ni kumpatia mkulima Soko na bei Nzuri"

"Tumeamua kuweka vituo katika wilaya ili kuwasogelea wakulima, hii ni badala ya makao makuu ya Mikoa kama ilivyokua awali, na pia tunaweza kuongeza Idadi ya vituo kutokana na mahitaji"

"Fikra na mipango ya Serekali katika kusimamia (stabilize) na kuwalinda (protect) wakulima.
Ndugu zangu hii ni sehemu tu, na sasa uwezo wetu wa kuhifadhi mazao pia umeongezeka."

"Mipango yetu ni kuendelea kuitumia NFRA kama wahifadhi wa chakula (food reserve) na Pia chombo cha kumlinda mkulima (stabilization instrument)."---- HUSSEIN BASHE

Post a Comment

0 Comments