MHE. DOROTHY ATOA UFAFANUZI WA CHANJO&DAWA ASILIA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dorothy Gwajima ametoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya dawa asilia na umuhimu wa chanjo kwa watu ili kuongeza kinga za miili yao.

Dkt. Gwajima amesema hayo leo akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na shughuli za Maendeleo ya Jamii Mkoani Mara.

Dkt. Gwajima amesema kuwa, pamoja na juhudi za kuelimisha umma kuhusu UVIKO-19 zinazoendelea, baadhi ya watu wasio waaminifu wanarudisha nyuma jitihada zinazofanywa na Serikali katika mapambano ili kuutokimeza ugonjwa huo.

Amesema matumizi ya tiba asili sambamba na huduma za chanjo inayoendelea kote nchini ni sehemu ya afua zinazohitaji elimu endelevu ili kuwezesha jamii kujikinga dhidi ya janga la UVIKO 19 linalousumbua ulimwengu.

"Hata darasani kwenye mtihani haiwezekani wanafunzi kupata A kwa pamoja ipo asilimia kama 30 ya wanafunzi watapata asilimia kubwa, darasa litaendelea kupata weingine asilimia 20, asilimia 20...asilimia nyingine inayobaki hata ukifanya nini, watabakia hivyo hadi tuition, hivyo hata suala la UVIKO 19, liko hivyo elimu lazima iwe endelevu" alisema.

Aliendelea kusema kuwa, tangu kuanza kwa UVIKO mwezi Januari, 2020 kuna mambo mengi yamejitokeza kuna baadhi ya watu kwa makusudi wanapotosha ukweli, kwa lengo la kuchafua hali ya hewa na kuharibu heshima na hadhi ya hayati aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati JPM.

"Kwanza mwaka jana wakati UVIKO unaingia nchini chanjo haikuepo, ... mtakumbuka hayati akiwa Chato alisema tutumie dawa asili kujifunza kama njia ya kujinusuru... nami nilitoa maelekezo kama Waziri wa Afya,...tiba ya asili ipo na ilikuwepo, inaendelea kutumika," alisema na kuongeza kuwa baada ya chanjo ya UVIKO 19 Serikali imejiridhisha na usalama wake hivyo kushauri wananchi kuanzia miaka 18 wajitokeze kuchanja ili kuongeza kiwango cha kinga ya mwili dhidi ya maradhi hayo.

Alifafanua kuwa, baadhi ya nchi ugonjwa wa UVIKO-19 umeanza kuwapata watoto na baadaye hali inaweza kuwa mbaya zaidi, hivyo kutoa rai kwa wananchi kuendelea kuwasikiliza Wataalamu wa Afya kwa kupata chanjo ili kuzinusuru afya zao.

No comments