KAGERA SUGAR NA SIMBA SC WAMALIZANA SWALA LA MHILU
Klabu ya Kagera Sugar imetangaza kukamilisha na kufikia makubaliano ya pande zote mbili (Kagera Sugar FC na Simba Sc) juu ya uhamisho wa aliyekuwa mchezaji wao Nyota Yusuph Valentine Mhilu kwa Dau la Tsh. 40M.
Yusuph Mhilu alisaini kandarasi ya miaka Miwili kuitumikia Kagera Sugar Football Club Mwaka Jana 2020.
Hivyo uhamisho huu wa Yusuph Mhilu kwenda Simba ni Uhamisho ambao umehusisha kuvunja Mkataba wake wa Mwaka mmoja uliosalia ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.
Kagera Sugar imemtakia kila la Kheri huko aendako na Mungu amsimamie katika kukiendeleza kipaji chake.
Post a Comment