HUKUMU YA KESI YA SABAYA NA WENZAKE OKTOBA MOSI
Hatua hiyo inakuja baada ya washtakiwa hao kumaliza kujitetea leo Jumanne Agosti 24, 2021.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na mawakili sita Dancan Oola,Mosses Mahuna, Edmund Ngemela, Sylvester Kahunduka, Fridolin Gwemelo na Jeston Jastine.
Upande wa Jamhuri ulioita mashahidi 11 ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, wakili Mwandamizi Abdalah Chavula, na Mawakili wa Serikali Felix Kwetukia na Baraka Mgaya.
Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, amesema Mahakama hiyo itatoa hukumu dhidi ya watuhumiwa hao Oktoba Mosi mwaka huu.
Hakimu huyo alikubali maombi ya mawakili wa pande hizo mbili walioomba kufanya majumuisho kwa njia ya maandishi kwa muda wa siku saba.a
Katika Kesi hiyo, Sabaya na wenzake wawili wanaotuhumiwa Kwa makosa matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika duka la Mohamed Saad lililopo eneo la bondeni jijini Arusha Februari 9 mwaka huu.
Post a Comment