HARMONIZE AIBUKIA KWENYE UIGIZAJI

Mwanamuziki Harmonize ameibukia upande wa uigizaji baada ya kutajwa kama moja ya wahusika wakuu (starring) katika movie ya A Life To Regret.

Kupitia kampuni ya BJB Films ambao ndio waandaaji wa filamu hiyo, imemtaja mkali huyo kutoka Konde Gang na nyota wengine wa Bongo Movie kama Patcho Mwamba, Stan Bakora, Nelly Kamwelu huku wasanii wengine kama H.Baba na Awilo Longomba wakijumuishwa pia kwenye movie hiyo inayotarajiwa kutoka siku za usoni.

Katika hili Harmonize anaingia kwenye orodha ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva walio ingia pia kwenye sanaa ya maigizo.

No comments