Msanii wa Muziki @officialzuchu kutoka katika Label ya WCB, ametangaza kuingia kesho Live kwenye kipindi cha Mashamsham Wasafi FM, kwa ajili ya kutambulisha wasanii watakao perfom kwenye stage ya Zuchu Home Coming.
Ametoa mtihani wakuotea wasanii watano, ambae atapatia atalipiwa Ndege kwenda na kurudi Hotel 5 Stars na atakaa kwenye Show 21/08/2021 Uwanja wa Amani mwaka mmoja na miezi mitatu kwenye Game.
"Naandaa event yangu ya kwanza mwenyewe kwenye uwanja Wow, Alhadulillah"
Aidha, amewataka mashabiki kukaa karibu na Radio akiwa kwenye kipindi cha Mashamsham ya Wasafi FM, akitangaza wasanii watakao perfom kwenye Show ya Zuchu Homecoming.
0 Comments