Aliekuwa Mtangazaji wa Habari, Michezo na Mchambuzi wa Magazeti Maulid Baraka Kitenge kupitia kituo cha Wasafi Media, ameacha kazi huku chanzo kikiwa bado hakijajulikana mpaka muda huu.
Aidha, Wasafi Media wametoa shukrani zao za dhati kwa Maulid Kitenge kwa kazi aliyoifanya mpaka kufikia kituo hicho kilipo.
"----->Kwanza kabisa nikushukuru kwa mchango wako mkubwa Katika taasisi ya Wasafi Media, kwa kuwa nasi bega kwa bega kuanzia Media changa mpaka leo imekuwa Media nambari moja Nchini katika kila report"
"Hakika haikuwa rahisi, shukran sana na sasa nina amani ukirudi nyumbani"
"Mbali ya ushiriki wako kwenye Media, siku zote umekuwa ni kama kaka ama Uncle kwangu na ninakuahidi kwenda kwa kasi ileile ambayo siku zote umenisihi kuifanya, ili kutimiza Malengo ya Wasafi Media kuwa chombo kikubwa cha Habari Africa na kulipa heshima Taifa letu."----> Mkurugenzi Mkuu (CEO) wa Wasafi Media, Diamond Platnumz.
0 Comments