AMKA NA BWANA LEO 31/08/2021

KESHA LA ASUBUHI

Jumanne 31/08/2021

 *SIRI YA UKUAJI WA KIROHO* 

*"Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu saba Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo"* *Waefeso 4:13*

*Iwapo tu wafuasi wa Kristo wangekuwa watafutaji kwa bidii wa hekima, wangeongozwa kwenye maeneo yenye kweli tele, ambazo bado hazijafahamika kabisa kwao*.Yeye ambaye atajitoa kwa Mungu kikamilifu kama alivyojitoa Musa, ataongozwa na mkono wa kiungu kama kweli ilivyokuwa kwa kiongozi mkuu wa Israel. 

*Anaweza kuwa wa hali ya chini na kuonekana kutokuwa na kipaji; lakini ikiwa kwa moyo wa upendo, wenye kutumaini atatii kila tangazo la mapenzi ya Mungu, uwezo wake utatakaswa, utaadilishwa,utaongezwa nguvu, na uwezo wake utaongezwa.* Kadiri anavyothamini sana masomo ya hekima ya kiungu, agizo takatifu litakabidhiwa kwake; atawezeshwa kuyafanya maisha yake kuwa heshima kwa Mungu na baraka kwa ulimwengu.

*Leo wengi hawajui kazi ya Roho Mtakatifu moyoni kama walivyokuwa wale waumini wa Efeso( angalia Matendo 19: 1-6 ); lakini hakuna ukweli uliofundishwa kwa uwazi zaidi katika Neno la Mungu kama huu*. Manabii na Mitume wameandika sana juu ya Mada hii. Kristo  mwenyewe  anatuelekeza kwenye ukuaji wa ulimwengu wa uoto kama kielelezo cha nguvu ya Roho wake katika kuhimili maisha ya kiroho.

Utomvu wa mzabibu, unaopanda kutoka kwenye mizizi, Unaenezwa kwenye matawi, kuhimili ukuaji na kutoa maua na matunda. Hivyo *nguvu ya Roho Mtakatifu itiayo uzima, inayotoka kwa Mwokozi, inaenea ndani ya roho, inafanya upya nia na mapenzi, na inaleta hata mawazo katika utii wa mapenzi  ya Mungu, na kumwezesha mpokeaji kuzaa matunda ya thamani ya matendo matakatifu*.

*Mtengenezaji wa maisha haya ya kiroho haonekani, na njia hasa ambayo kwayo maisha hayo hugawiwa na kuendelezwa, iko nje ya Uwezo wa falsafa ya wanadamu kuelezea.* Kama ilivyo katika ulimwengu wa asili, ndivyo ilivyo katika Ulimwengu wa kiroho.Uhai wa kawaida unahifadhiwa kila wakati na nguvu za kiungu; lakini bado hauendelezwi na muujiza wa moja kwa moja, bali ni kupitia matumizi ya baraka zilizowekwa karibu nasi.

*Hivyo uhai wa kiroho unaendelezwa na matumizi ya njia ambazo Mungu ametoa. Ili mfuasi wa Kristo  apate kukua "hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo"( Waefeso 4:13), ni lazima ale mkate wa uzima, na kunywa maji ya wokovu.*

*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI MPENDWA*

No comments