AMKA NA BWANA LEO 26
*KESHA LA ASUBUHI.*
Alhamisi, 26/08/2021.
*JIHADHARINI NA USHIRIKINA.*
*Na Wakati wanapokuambia, tafuta habari Kwa watu wenye pepo na kwa wachwi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende Kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Isaya 8:19.*
▶️Umizimu ndio kazi bora kabisa ya udanganyifu. Ndio madanganyo ya shetani yaliyofanikiwa mno na yenye kuvuti sana - ambayo yamekusudiwa kuvuta huruma za wale ambao wamewalaza wapendwa wao kaburini. Malaika waovu huja Katika maumbo ya wale wapendwa, na kusimulia visa vinavyohusiana na maisha yao, na hufanya matendo ambayo waliyatenda walipokuwa wanaishi. Kwa njia hii wanaowaongoza watu kuamini kwamba marafiki wao waliokufa ni malaika, wanaozunguka juu yao, na kuwasiliana nao. Malaika waovu hawa, ambao wanajifanya kuwa marafiki waliokufa, huheshimiwa Kwa ibada fulani ya sanamu, n kwa wengi neno lao Lina uzito mkubwa kuliko neno la Mungu. Hivyo wanaume na wanawake wanaongozwa kukataa ukweli, "wakisikiliza Roho zidanganyazo."
▶️Neno la Mungu linatangaza kwa maneno chanya kwamba "walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui Neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; Wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua" (Mhubiri 9:5, 6). Andiko hili dhahiri linapingana moja kwa moja na mafundisho ya Umizimu, na kama lingesikilizwa lingeokoa roho kutokana na mtego wa adui.
▶️Wengi wanauchunguza umizimu kwa sababu tu ya udadisi. Hawana imani ya kweli ndani yake, nao wangeanza kurudi nyuma kwa kutishwa na wazo la kuwa chombo cha mawasiliano na mizimu; Lakini wanathubutu kuingia kwenye ardhi iliyopigwa marufuku na ya hatari. Wanapokuwa imara katika kazi ya yule mdanganyifu, wanajikuta wako Katika mamlaka ya yule anayefanya watumishi wake kuwa watumwa duni kabisa, na hakuna kinachoweza kuwaokoa isipokuwa nguvu ya Mungu. Usalama pekee kwetu ni kutumainia kabisa na kufuata kwa uaminifu mafundisho ya Neno la Mungu. Biblia ndiyo ramani pekee inayoonesha njia nyembamba ambayo inaepuka mitego ya uharibifu ....
▶️ *Ni upendo ulioje, ni upendo wa ajabu kiasi gani, kwamba Mungu anavumilia upotovu wa watu wake, na hutuma msaada kwa Kila nafsi inayotamani kufanya mapenzi yake, na kuacha dhambi! Iwapo tu mtu atashirikiana na mawakala wa Mbinguni, anaweza kufanikiwa zaidi kuwa mshindi. Viumbe walioanguka kama tulivyo, wenye uwezo wa uhalifu wa kuchukiza kabisa, lakini bado tunaweza kuwa washindi.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment