AMKA NA BWANA LEO 2

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumatatu, 02.08.2021.

*YESU, RAFIKI YAKO MAHAKAMANI.*

*Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16.*

▶️Tunapokuwa na ahadi yenye nguvu na kamili kama[Yohana 3:14-19]... Ninauliza, "Je ni udhuru gani alio nao yeyote kati yetu kwa ajili ya kutokuamini? Una udhuru gani wa kutokusema, " Sidhani kama Bwana anasikia maombi yangu; Ninatamani kama ningeamini kuwa mimi ni Mkristo, au ninatamani kama ningekuwa na ushahidi kwamba mimi ni mtoto wa Mungu"? Hisia zinabadilika sana, lakini hapa kuna maneno yenye thamani kubwa ya uzima wa milele.

▶️Ushahidi ni nini? Je, ni kupita haraka kwa hisi? Je, ni mhemko wa moyo ambao ndio unakupa ushahidi kwamba wewe ni mtoto wa Mungu? Lakini hapa kuna neno lenye thamani kubwa la uzima wa milele nalo linatupa uthibitisho kwamba tunaweza kushikilia tumaini lililowekwa mbele yetu katika injili kwa imani hai.

▶️Tunaweza kumwendea Yesu Kristo ambaye ni mtetezi wetu katika nyua za mbinguni. Tunamhitaji rafiki mahakamani. Tumekuwa tukitenda dhambi, tukikosa kuwa watiifu, wavunjaji wa sheria, na ni jambo lenye umuhimu wa juu kabisa kwetu kwamba tunaye  Rafiki mahakamani wa kutetea kesi zetu mbele ya Baba. Anasema, "Nikiinuliwa nitawavuta wote kuja kwangu." Sawa, je  wote watavutwa? Kristo anavuta lakini je watakubali kuvutwa kwake? Je watakuja? Wito hapa katika Ufunuo ni kwamba: "Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure." (Ufunuo 22:17).

▶️Si mchungaji pekee anayepaswa kusema, "Njoo," bali hebu yeye asikiaye na aseme, "Njoo." Ndipo itakubidi kusikia kwa kusudi, na unaposikia ujumbe unaanza kuusema, nawe unasema, "Njoo." Kwako kule kuja ndiko kila kitu. Na kadiri unavyoona kwamba unaweza kuja, faida ni kubwa mno, usiyoistahili kabisa, kiasi kwamba unajisikia kwamba ungependa kila mtu kuipata faida pamoja nawe, hivyo tuwe na watendakazi pamoja na Mungu. Hii ndio kazi yetu.

▶️ *Mungu anasema, "Njoo," Roho anasema, "Njoo," Bwana arusi anasema, "Njoo," na kila asikiaye na aseme, "Njoo." Ndio, ili kwamba wengi kwa maisha thabiti ya utauwa na kwa maneno ya vinywa vyao waseme, "Njoo." ... Siyo kwa amri peke yake, bali kwa mfano unaouonesha unabeba kielelezo hai pamoja nawe kwamba mbinguni ni pazuri, kwamba Ukristo unastahili kuhangaikiwa.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

No comments