AMKA NA BWANA LEO 1/09/2021


KESHA LA ASUBUHI

Jumatano 01/09/2021

*POKEA ILI UPATE KUTOA*

*"Basi yeye apandaye na yeye atiaye maji ni wa moja, lakini kila mtu atapata thawabu yake Mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe."*
*1Wakorintho 3: 8*

*Kristo alipowaita wanafunzi wake kutoka kwenye nyavu zao za kuvulia samaki, aliwaambia kwamba walipaswa kuwa wavuvi wa Watu. Kwa hili Kristo alimaanisha kwamba walipaswa kufanya kazi.* Katika kuwasilisha ukweli kwa wengine,walipaswa kutupa nyavu zao upande wa kulia wa meli. Kwa hili Kristo alimaanisha kwamba walipaswa kufanya kazi kwa imani katika kuokoa roho. Na kazi hii kwa watu binafsi ingeweza, kwa majaaliwa ya Mungu, kuwaongoza kufanya kazi kwa ajili ya jamii,hawakupaswa kujifikiria wenyewe kuwa sehemu ya  mifumo tofauti ya kazi, bali nyuzi moja moja za kitu kizima kikubwa,zilizounganishwa kwa namna isiyoweza kutenganishwa kama viungo kwenye mnyororo,wakiunganishwa na wanadamu wenzao pia na Mungu.

*Mungu anataka sana Vijana kuwa stadi, wachapa kazi, wakivaa nira ya Kristo, wakibeba mizigo Yake. *"Ninyi ni watenda kazi pamoja na Mungu"* anasema Watoto pamoja na Vijana wanapaswa  kutafuta kwa bidii kabisa kusonga mbele katika ufahamu, katika Upataji wa akili kwa kujifunza; lengo lao linapaswa kuwa katika mambo ya Kiroho na yale ya maisha haya pia, ili kufanya kazi katika mpango wa kuongeza.

 " Mkijitahidi sana"  mtume Petro anasema, *"Katika Imani yenu tieni  na wema, na katika Wema wenu Maarifa; na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika maarifa yenu kiasi,na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu,na katika upendano wa ndugu  upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo"( 2Petro 1:5- 8)*

Maendeleo katika elimu ya Kweli hayapatani binafsi. *Maarifa ya Kweli  hutoka kwa Mungu,  na hurudi tena kwa Mungu Watoto wake wanapaswa kupokea ili wapate kutoa tena*.Wale ambao kupitia neema  ya Mungu wamepata faida za kiakili na za kiroho wanapaswa,  kadri wanavyosonga mbele, kuwavuta wengine pamoja nao kufikia ubora wa juu  zaidi. Na kazi hii iliyofanywa katika kukuza kufaa kwa wengine,itakuwa na ushirikiano wa mawakala wasioonekana.

*Kadiri tunavyoendelea na kazi hiyo kwa Uaminifu, tutakuwa na matarajio ya juu kwa ajili ya haki, utakatifu, na maarifa kamili kuhusu Mungu. Sisi wenyewe tutakamilika katika Kristo katika maisha haya, na tutachukua kwenda nao katika nyua za juu uwezo Wetu ulioongezeka, ili kuendeleza elimu yetu ya juu zaidi huko.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*

No comments