UNABII SIKU YA MWISHO

#UNABII WA #MIAKA 6000.
#MIAKA 2000 YA #MWISHO.
TOKA #KIFO CHA #YESU MSALABANI #MWAKA 31.5AD HADI #ANAPORUDI MARA YA PILI.

BWANA AWABARIKI.

 Mwenye sikio na asikie, mwenye kuelewa na aelewe.

Leo mpenzi msomaji tunamalizia sehemu ya mwisho ya unabii huu makini kabisa wa miaka 6000, katika kipengele cha miaka 2000 ya mwisho yani kutoka 31.5AD YESU alipokufa msalabani hadi anaporudi mara ya pili.

Daniel 9:2, 
Mimi Daniel kwa kuvisoma vitabu , nalifahamu hesabu ya miaka ambayo neno la BWANA lilimjia yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa yerusalemu yaani miaka sabini.

Ni kwa kuvisoma vitabu tulivyopewa na BWANA yani BIBLIA na vitabu vya Roho ya unabii tu, ndipo tutaweza kutambuwa  kuwa ukombozi wetu umekaribia. Tutaijuwa miaka ambayo YESU anakaribia kuja. Ila siku na saa hatutaijuwa hadi pale MUNGU atapoitangaza rasmi kwenye kipindi cha ufufuo maalumu.

Basi turejee kwenye unabii wa KRISTO kwa adamu.

👉🏻Hivyo kwa Adamu yalifunuliwa matukio muhimu katika historia ya mwanadamu , kutoka ambapo kauli ya MUNGU ilitangazwa edeni, hata katika gharika na kuendelea hadi ujio wa kwanza wa YESU . Alionyeshwa kwamba wakati kafara ya KRISTO ingekuwa yenye thamani ya kutosha kuokoa ulimwengu mzima , wengi wangechagua maisha ya dhambi kuliko toba na utii. #Patriarchs & Prophets . P 67.3

Tumekwisha kuona tangia edeni hadi gharika , toka gharika hadi kifo cha YESU msalabani mwaka 31.5AD. 

👉🏻Sasa leo tutaangalia kuanzia msalabani hadi mwisho wa historia ya dunia/hadi YESU anaporudi.

Zaburi 90:1-2, 9-13

BWANA alipotamka hukumu kipindi cha Nuhu aliapa kuwa miaka ya mwanadamu itakuwa ni miaka 120 tu, hivyo BWANA alimaanisha zaidi ya swala la umri, BWANA alimaanisha kwamba kikombe chao cha uovu kinakaribia kujaa, na baada ya miaka 120 kikombe cha uovu kilijaa na waovu wote wakakinywea kwa gharika ya maji.

Daudi naye akasema, siku za miaka yetu ni miaka 70 na ikiwa tuna nguvu ni miaka 80 nayo imejaa taabu na ubatili. Daudi asema, Ee BWANA utufundishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima.

Wakati wetu uko mikononi mwa MUNGU , kila mda ni wake, tuko chini ya wajibu mkuu kuutumia vyema kwa utukufu wake, hakuna taranta ambayo atadai tutoe hesabu kuliko hii ya mda wetu.  Thamani ya mda inapita mahesabu. The Faith I Live By p 158.3

Miaka 70 au 80 ambayo BWANA alimvuvia daudi, EGWhite anasema, tuna siku tu chache za mlango wa rehema.

Huu mlango wa rehema unaotajwa kwenye hiyo nukuu ni mlango wa rehema wa mtu mmoja mmoja katika ulimwengu huu. Umri wa mwanadamu uliendelea kushuka miaka 70 hadi 80 na wengine hawaifikii. Tunapokufa tu mlango wetu wa rehema unafungwa.

Leo wanadamu hawajui kuzihesabu siku zao. Wakati wa kuvunjwa kwa Yerusalem kulikuwa na watu hawajui kuzihesabu siku zao. Na katika wakati huu wa mwisho Yesu asema.

Mathayo 24:37-38

Anasa za siku za nuhu ndizo anasa za watu wa leo wanaoenda kufunga historia ya dunia hivi punde. Watu ni wakaidi mno mpaka makanisani humu tunamoabudia. 

Kila baada ya miaka 2000 kikombe cha uovu duniani kinajaa.

Miaka 2000 ya kwanza kikombe cha uovu kilijaa na waovu walikinywea kwa gharika siku za nuhu.

Miaka 2000 ya pili ilipotimia katika ule mwaka wa 31.5AD kikombe cha uovu kilijaa, YESU akakinywea badala yetu sisi waovu.
             Mathayo 26:39
                     Yohana 3:16

Baada ya kuwa YESU amekinywea kikombe cha adhabu ya Wanadamu katika ile miaka 2000 ya pili, sasa kikombe cha uovu wa Wanadamu kinajaa tena kwa hakika.

YESU alitoa ombi kwa wanafunzi wake wawe na umoja hadi mwisho wa dunia. Yohana 17:1-26

E. G. White anasema,

Ombi la KRISTO siyo tu kwa wale ambao ni wanafunzi wake hata sasa, bali na wale watakaoamini kupitia neno la wanafunzi wake hata mwisho wa dunia. YESU alikuwa karibu kujitoa uhai wake ili kuleta uzima na kutokufa katika nuru. KRISTO kati ya mateso yake na kule kukataliwa kila siku na Wanadamu , alitazama mbele ya mstari wa miaka 2000 kwa kanisa lake, ambayo ingekuwaki katika siku za mwisho kabla ya kufungwa kwa historia ya dunia. #Manuscript Releases Vol 1. P 355.1

E. G. White alionyeshwa miaka 2000 mingine ndipo historia ya dunia itafungwa.👆🏻👆🏻👆🏻

👉🏻Kisha kutakuwa na sheria Dhidi ya Sabato uumbaji wa Mungu, na kisha Mungu atatenda kazi yake ya kutisha juu ya dunia. Amevumiliana na uovu wa wanadamu, amewajaribu kuwaongoa warudi kwake, lakini muda unakuja ambapo watakuwa wamekijaza kikombe cha uovu, na kisha MUNGU atatenda. Wakati huo karibu umefikiwa. MUNGU huweka kumbukumbu za mataifa, namba zinazidi kuongezeka dhidi yao katika vitabu vya MBINGUNI , na pale itakapokuwa sheria, uasi wa siku ya kwanza ya juma(jumapili) utaambatana na adhabu, kisha kikombe chao kitakuwa kimejaa. The Review and Herald , march , 9, 1886
7BC p 910.5

Katika kizazi hiki dharahu kubwa kuliko huonyeshwa kwa MUNGU . Kikombe cha maovu karibu kinajaa. That I May Know Him. p 355.2

Neno la Mungu kupitia manabii wake linasema, kikombe cha uovu karibia kinajaa. Na wakati huo uko karibu.

👉🏻Katika kila kujaa kwa kikombe cha uovu kulikuwa na kikomo cha miaka 2000. Na kulikuwa na uasi wa sheria ya sabato, ibada ya miungu, mauaji, kuchafuliwa kwa utaratibu wa ndoa, kuoana kwa watunza sabato na wapagani kinyume na maagizo ya MUNGU .

👉🏻Yesu alikuwa karibu kujitoa uhai wake ili kuleta uzima na kutokufa katika nuru. Kristo kati ya mateso yake na kule kukataliwa kila siku na wanadamu , Alitazama mbele ya mstari wa miaka 2000 kwa kanisa lake ambayo ingekuwa katika siku za mwisho kabla ya kufungwa kwa historia ya dunia. #Manuscript Releases Vol 1. 355.1

Kumbuka hiyo sentesi👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

JE, NI LINI YESU ALIJITOA UHAI WAKE ILI KULETA UZIMA???
............................................................................

👉🏻UNABII unasema kuwa, miaka hiyo 2000 itakayokuwako katika siku za mwisho kabla ya kufungwa historia ya dunia.

👉🏻Shetani anaweka mpango wake wa haraka kwaajili ya Pambano kuu la mwisho, wakati wowote watachukua upande wao. Baada ya injili kuwa imehubiriwa ulimwenguni kwa takribani miaka 2000, Shetani atawasilisha kwa wanaume na WANAWAKE matukio yale yale ambayo aliyawasilisha kws KRISTO . Kwa namna ya ajabu amefanya falme za ulimwengu  katika utukufu wake kupita mbela yao. Hizi huwaahidi wote ambao wataanguka kumsujudia, hivyo anatafuta kuwaleta wanadamu chini ya himaya yake.
#Testimonies for the church . Vol 6 p14.2

Rafiki, nikuambie, 👉🏻Tangu injili ianze kuhubiriwa toka Yesu alipofufuka hadi leo ni takribani miaka 1990, karibu kabisa na miaka 2000. Injili ilianza kuhubiriwa na mitume baada tu ya YESU kufufuka mwaka 31.5AD, maana yake ni kwamba karibia miaka 2000 itimie ambayo YESU aliiona kuwa itakuwepo kabla ya kufungwa kwa historia ya ulimwengu . Tutaangalia kwa kufanya hesabu rahisi.

BAADHI YA MATUKIO YATAKAYOASHIRIA KUWA KIKOMBE CHA UOVU KINAJAA.
.........................................................................

Kama ilivyokuwa siku za nuhu, ukengeufu ulitangulia kisha uharibifu ukafuata.

👉🏻Lazima kwanza kikombe kijae, na mtu wa kuasi kujiinua juu ya MUNGU na hata kuabudiwa. Wakati dunia inapoungana ili kumfanya mtu fulani kuwa kama Baba Mtakatifu, yani papa wa roma, atakaposhika hatamu za kuiongoza dunia kwa sheria ambayo itaiinuwa ibada ya Shetani , na serikali zote za dunia kuipa nguvu taasisi hii ya upapa, utakapoona jambo hilo ujuwe kikombe kimejaa. Hata hivyo mambo yako mbioni kukamilika.

Uasi mwingine ni uharibifu wa ndoa, ndoa za jinsia moja kuhalalishwa na serikali za dunia hii.

Uasi mwingine ni WASABATO kuoana na wapagani na kisha kukubaliwa kuwa ni ndoa katika mabaraza ya kanisa.

Uasi mwingine ni uvunjifu wa sabato. Sabato kuvunjwa kisheria na watu wa MUNGU  kuwekwa chini ya kongwa la rumi ya kidini mara ya pili.

👉🏻Je rafiki wajuwa kuwa nchi nyingi zilishaharalisha ushoga, ndoa za jinsia moja?? Ndiyo naamini unajuwa. Sasa unapoona mambo hayo yanapoingia hadi kwa wana wa MUNGU , hiyo ni ishara kuwa miaka 2000 inakaribia kuisha.

👉🏻1TM p 11.2
Katika siku za mwisho ili kujuwa kwamba miaka 2000 iko karibu, harakati za uovu zitakuwa za haraka zaidi.

Yani mambo yaliyo kinyume na maadili mema yatasukumwa kisheria na kukubaliwa na jamii yakiongozwa na viongozi wa dunia hii ambao ni mawakala wa Shetani .

Kama watu wa MUNGU tukiona mawakala wa shetani wako kasi sana katika kutimiza ajenda za shetani, ujuwe miaka 2000 inakaribia kuisha, sababu ni moja, mfalme wa uovu anayekuja mwishoni ni sawa na mtoto MAHEL-SHALAL-HASH-BAZ.

Ufunuo 17:11
Huyu mnyama anayejirudia hapa ni mmoja wa falme 7 zilizowahi kutawala dunia. Ila anajirudia naye yuko kasi kuenenda kwenye uharibifu, ndio maana harakati za mwisho za uovu leo ziko kasi mno sababu miaka 2000 ya mwisho imekaribia.

SASA TUANGALIE HESABU RAHISI KUTAMBUA KUWA MIAKA 2000 YA MWISHO ITATIMIA MWAKA GANI.
..........................................................................

WAADVENTISTA Wasabato wengi na wasio waadventista Wasabato wanadhani ya kwamba miaka 2000 ilishapita/timia na sasa tunaishi miaka ya rehema. Hili siyo kweli. MUNGU hawezi kukubali waovu watembee katika miaka ya millenium ya SABATO bila kuwaadhibu. Hilo litakuwa sawa na MUNGU kuruhusu wasabato kuvunja Sabato katika masaa ya sabato takatifu.

👉🏻Fuatana nami hapa👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Yesu alikufa msalabani mwaka 31.5AD
YESU alipaa MBINGUNI mwaka huo wa 31AD
Mitume wa YESU walianza kuhubiri injili mwaka wa 31AD

👉🏻👉🏻Sasa iko hivi👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Mwaka 31AD hadi mwaka 100AD= na miaka 69
Mwaka 100AD hadi mwaka 321AD= na miaka 221.

Mwaka 321AD hadi mwaka 538AD= na miaka 217

Mwaka 538AD hadi mwaka 1798= na miaka 1260.

Mwaka 1798 hadi mwaka 1844= na miaka 46

Mwaka 1844 hadi mwaka 2021= 177

👉🏻👉🏻👉🏻Sasa Jumlisha hiyo miaka kutoka mwaka 31AD hadi mwaka huu wa 2021.

69+221+217+1260+46+177 = na miaka 1990.

Ina maana kuwa tangu YESU apae kwenda mbinguni mwaka 31AD na injili kuanza kuhubiriwa duniani kote  hadi leo mwaka 2021, tayari injili imetimiza miaka 1990 tangu ihubiriwe, na  Yesu ametimiza miaka 1990 tangu kifo chake msalabani na kufufuka na akaenda mbinguni.

👉🏻👉🏻Toka mwaka 31AD hadi 👉🏻👉🏻mwaka 2021👉🏻👉🏻Tuna miaka 1990.

Je, miaka 2000 itafika lini tangu YESU aondoke na injili kuanza kuhubiriwa duniani kote toka mwaka 31AD?

Leo ni mwaka 2021, tangu YESU aondoke na injili kuhubiriwa tuna jumla ya miaka 1990.

Je, miaka 1990 bado miaka mingapi kufika miaka 2000??

👉🏻👉🏻1990+10 = 2000

Kwa hiyo bado miaka 10 tu ili miaka 2000 itimie Live.

Hivyo hesabu yetu itakuwa hivi👇🏻👇🏻👇🏻

👉🏻👉🏻Leo mwaka 2021 tumeona tuna miaka 1990 toka mwaka 31AD.

👉🏻Hivyo ni 2021+10 = 2031

👉🏻👉🏻Hivyo miaka 2000 ya mwisho itatimia vizuri kabisa mwaka 2031 katikati ya mwaka ule wa kiyahudi tangu YESU alipotulipia deni letu na tangu injili ianze kuhubiriwa duniani kote.

Rafiki, mimi na wewe hatujui yaliyo mbele yetu. Lolote laweza kutokea, mimi nimekufikishia ujumbe. Nani ajuaye katika hii miaka iliyobakia🤔, huenda mvua za masika zikamwagwa kwa watu wa MUNGU wanaojari unabii, huenda mlango wa rehema ukafungwa kwa waadventista Wasabato wote, au kwako au kwangu kwa njia ya kifo, huenda amri ya jumapili ikatangazwa kisheria duniani kote, ni nani ajuaye rafiki 🤔.

Hakika mda umekwisha. Neno la MUNGU linasema, hakuna aijuwaye siku wala saa, halijasema miaka. Miaka ambayo BWANA wetu YESU anakaribia kuja, hiyo MUNGU anatujulisha ili tujiandaye, ila siku na saa hajatufunulia bado.

Ni mimi mjoli mwenzenu. Pambano Ibrahim chindema.

No comments