TFF KUGAWA BARAKOA BURE LEO KWENYE DERBY

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuchukua tahadhari zote za Covid19 katika mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) Simba SC na Young Africans utakaochezwa leo Jumapili Julai 25, 2021 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

TFF imepanga kugawa bure Barakoa kwa kila mtazamaji atakayeingia kutazama mchezo huo utakaochezwa kuanzia saa 10 jioni.

Imesisitiza watazamaji kuchukua tahadhari zote za Covid19 ikiwemo kuvaa Barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka ambayo yatakuwepo katika maeneo yote ya kuingilia uwanjani.

No comments