SOKA LA ZANZIBAR LAZIDI VITUKO, TIMU YASHINDA 50-0
Jana katika Michezo ya mwisho ya kuitafuta timu moja itakayopanda Daraja la Kwanza Kanda Unguja kutoka Ligi ya Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo Mchezo nambari 113 ulichezwa katika Uwanja wa Mau B timu ya Umoja wa Mbuzini ilishinda jumla ya mabao 50-0 dhidi ya New City na mchezo mwengine nambari 114 uliochezwa uwanja wa Mau A timu ya Kundemba ilishinda mabao 46-0 dhidi ya Muungano Rangers.
Kwanini wakafungana idadi hiyo ya mabao?
Hatua hiyo ilikuwa ni 4 bora inatafutwa timu 1 itakayopanda daraja la kwanza kutoka Mkoa, kabla ya mechi hizo za mwisho ambapo Kundemba ilikuwa inaongoza hatua hiyo ikiwa na alama 4 na mabao 2 ya akiba sawa na Umoja ya Mbuzini yenye alama 4 pia lakini ina bao 1 la akiba, hivyo Kundemba na Umoja wa Mbuzini ndizo timu pekee zilizokuwa na tamaa ya kupanda daraja na kila timu ilihitaji ishinde ili ipande, lakini akili zao kwa vile michezo yote imechezwa wakati mmoja na Viwanja vya karibu yani Mau A na B basi ikapelekea idadi ya mabao kuongezeka kwa maana likifika bao la 10 uwanja wa pili wanaambiwa huku linaingia la 11, wakifika la 11 kule linaaingia la 12 na ikaenda hivyo mpaka kufika idadi hiyo ya mabao
Kwa mujibu ya Kanuni ya Mashindano ya Soka Zanzibar Msimu wa mwaka 2020-2021 zile timu zilizoachiana jana kwenye Ligi ya Mkoa wa Mjini Magharibi huenda zikapewa adhabu hii.

Post a Comment