SERIKALI KUTOA USHIRIKIANO NA TAMASHA LA ZIFF
Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mazungumzo na uongozi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ukiongozwa na Mkurugenzi wake Profesa Martin Muhando.
"Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Nane itaendelea kutoa ushirikiano wake katika kuhakikisha Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) linaendelea kupata mafanikio zaidi" ---- MWINYI
Aidha, Rais Hussein Mwinyi amesema, kuna haja ya kuanzishwa kwa vyuo vya kuzalisha vipaji katika tasnia ya filamu nchini ili kuwawezesha vijana sambamba na kuwaunganisha pamoja ili waweze kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Post a Comment