POLISI TANZANIA YAACHANA NA WACHEZAJI WAKE 13
Klabu ya Polisi Tanzania imeachana na wachezaji wake 13 baada ya Mikataba yao kwisha na klabu kufikia uwamuzi wa kutokuongeza mikataba ya
kuendelea nao tena kwa msimu ujao.
Wachezaji ambao hawataonekana kwenye msimu ujao wakikitumikia kikosi cha Polisi Tanzania kwenye michezo ya Ligi Kuu na ya Mashindano mengine ni:-
01. MARCEL KAHEZA
02. MOHHAMMED BAKARI
03. MOHAMMED YUSUPH
04. MOHAMMED KASSIM
05. RAMADHANI KAPELE
06. PATO NGONYANI
07. PIUS BUSWITA
08. JIMMY SHOJI
09. JOSEPH KIMWAGA
10. GEORGE MPOLE
11. EMMANUEL MANYANDA
12. ERICK MSAGATI
13. HASSAN NASSORO ZANIA
Klabu inawashukuru kwa mchango wao kwa kipindi chote walichokuwa wakiitumikia Polisi Tanzania na inawatakia heri katika maisha yao mapya wakiwa nje ya Polisi Tanzania.
Pia Klabu ya Polisi Tanzania imependa waleweke kuwa, hakuna mchezaji ambaye anaondoka kwao kati ya hawa ambaye klabu ilikuwa bado ipo kwenye mipango nae, isipokuwa wote walioachana nao kwenye timu yao, klabu ilionahuduma waliyotupa imefika kikomo baada ya mikataba yao kwisha na hakuna sababu ya kuongeza nao mikataba na kuwaacha
waende wakatafute changamoto nyengine.
"Aidha, Klabu imewarejesha wachezaji wote waliokuwa wamekuja kwetu kwa mkopobkwenye vilabu vyao baada ya msimu kumaliza"
"Kuelekea msimu mpya tunaingia sokoni sasa katika kusuka upya kikosi chetu kwa kuongeza sura mpya zisizozidi 8 na tutaendelea kubaki na wachezaji 19 waliokuwa nasi kwa msimu uliopita."---- POLISI TZ
Post a Comment