RAIS WA MPITO MALI, ASSIMI GOITA ANUSURIKA KUCHOMWA KISU

Wanaume wawili wamejaribu kumdunga kisu Rais
wa mpito wa Mali Assimi Goïta katika msikiti uliopo katika mji mkuu, Bamako.

Kanali Goïta allikuwa akihudhuria ibada ya siku ya
Eid al-Adha katika msikiti wa Grand Mosque.

Mafisa wanasema washambuliaji, ambao kwa
mujibu wa Shirika la habari la AFP walikuwa ni
wawili, wamekamatwa na rais ameondolewa kwenyebmsikiti huo kwa usalama wake.

Haijafahamika iwapo Kanali Goïta, ambaye
aliongoza jeshi kuchukua mamlaka mwezi Agosti,
alijeruhiwa.

Mkurugenzi wa msikiti aliliambia shirika la habari
kwamba mtu alimlenga waziri lakini alimjeruhi mtu mwingine.

No comments