SERIKALI YAPELEKA BILIONI 20.3 HALMASHAURI 34

Upelekaji wa Huduma za AfyaMsingi kwa Wananchi: Serikali imepeleka kwenye Halmashauri 34 kiasi cha Shilingi bilioni 20.3 kwa ajili ya kuendelea na Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri 34 ambapo ujenzi unaendelea.

Halmashauri 76 zimepelekewa fedha kiasi cha Shilingi bilioni 11 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati 3 kila Halmashauri hivyo Jumla ya Zahanati 228 zitakamilishwa.

Vilevile, Kupitia mradi wa matokeo ya ufanisi (Result Based Financing -RBF) umefanyika uboreshaji wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya ambapo Zahanati 279, Vituo vya afya 46 na hospitali 22 za Wilaya zimepatiwa fedha kiasi cha Shilingi bilioni 30.8 ili kuviwezesha vituo hivyo kufika ngazi ya nyota tatu katika ubora wa utoaji huduma.

Kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya kiasi cha Shilingi 1.6 zimetolewa kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya usingizi katika vituo vya afya 32 ili kuviwezesha vituo hivi kufanya upasuaji ikiwemo upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni.

Kupitia Mradi wa Commodity Import Support, Serikali imewezesha ujenzi wa Vituo vya afya 20 katika Halmashauri 20 na kila Kituo cha afya kimepatiwa kiasi cha Shilingi milioni 500. Lengo la ujenzi wa vituo vya afya ni kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kupunguza vifo hususani vinavyotokana na uzazi.

Serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya, ndani ya Siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan Serikali imeajiri watumishi 2,726 wa afya wakiwemo madaktari, wauguzi na watalamu wa maabara na kuwasambaza katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri.
Mhe. Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI 06.07.2021

No comments