SABABU KESI YA OLE SABAYA KUPIGWA KALENDA
SABABU YA KESI HIYO KUHAIRISHWA;
Kesi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake watano wanaokabiliwa na mashtaka sita yakiwemo mawili ya ujambazi wa kutumia silaha imeahirishwa hadi Julai 16, 2021.
Juni 18, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Sabaya na wenzake wawili walisomewa mashtaka mawili na leo Ijumaa Juni 2, 2021 ndio ilikuwa siku ya mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao lakini ikaelezwa kuwa hawapo.
Siku hiyo ilielezwa kuwa Februari 9, 2021 katika mtaa wa Bondeni, Sabaya akiwa na watuhumiwa wenzake wawili walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kuvamia duka la Said Saad na kuwaweka chini ya ulinzi.
Ilielezwa kuwa Sabaya na walinzi wake, Sylivester Nyingu (26) maarufu Kicheche na Daniel Mbura(38) walitenda kosa hilo baada kumfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetini na kumuibia 390,000.
Katika tukio hilo wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao pia wanatuhumiwa kumpiga mateke kumtishia silaha na kumpora simu na Sh35,000 Ramadhani Ayoub. Watuhumiwa hao ambao walikana mashtaka yanayowakabili wanatetea na wakili, Moses Mahuna.
Leo katika mahakama hiyo ilidaiwa mashtaka mengine manne yanayowakabili upelelezi wake bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Tarsila Garvas aliomba kupangwa siku nyingine ili mashahidi hao waanze kutoa ushahidi wao na hakimu mkazi mkuu, Salome Mshasha alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 16, 2021.
Post a Comment