NENO KUU MAKAMBINI LEO 1
SOMO: KUANZA MWENDO NA KUMALIZA MWENDO.
Pr. Godwin Lekundayo
Makambi-Tanga Jiji
Trh 01 July 2021
👂1 Wakorintho 10:1-6
✓Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
✓wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
✓wote wakala chakula kile kile cha roho;
✓wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
✓Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
✓Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
👂Paulo anataka tufahamu kuwa babu zetu walipita chini ya wingu na bahari
👂Lengo la Mungu lilikuwa ni kuwatoa wana wa Israel misri waelekee kaanani ...na tunaambiwa kuwa hata baadhi ya wamisri walijiunga nao.
👂Kumbuka baada ya kuwa wamevuka mto yordani Walishangilia kwa ushindi mkuu na hata akina mariam wakatunga nyimbo , chakushangaza walifikia mahari wakasahau makuu ya Mungu na kuanza kumnung'unikia musa.
👂 Mungu alikasirika kiasi cha kuwaangamiza wana wa Israel...lkn Musa alisimama kwa ujasiri akimwambia Mungu kama unataka kuwaangamiza hawa wote naomba unifute katika kitabu cha uzima. Nae Mungu akakubali ombi la Musa.
👂Wakafika mahali wakamlilia musa eti wanataka nyama nae musa akamwambia Mungu .....gafla Mungu akawaaletea kwale wakala nyama adi zikawatokea puani
👂Tazama pia musa anaambiwa auamru mwamba utoe maji....lkn kwa sababu alikuwa amechanganywa mafaili kutokana na manyanyaso ya wana wa Israel akasahau maagiza hatimae akaupiga mwamba mara 3 na ukatoa maji. Ni vizuri ujifunze kusikiliza Roho Mtakatifu anasemaje, usitumie uzoefu wako kufanya kitu chochote kile.....(ujue hata musa alitumia uzoefu wake akaupiga mwamba).
👂Acha Roho aongoze na tuzitumie mazoea kuendesha mambo.
👂Mwamba huo ulikuwa ni YESU KRISTO...pia tambua kuwa wana wa Israel walibatizwa kama sisi kwani walipita katika mto wa Yordani.
👂Kwa maana hiyo Mungu wetu ana msimamo katika utendaji wake alimwambia musa kuwa ametenda kosa na Mungu wetu sio kigeugeu ...Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
👂Pamoja na kula kwao pasaka, kubatizwa Mungu hakupendezwa nao....maana Mungu aliruhusu watu 2 kwenda kaanani je wengine walikuwa wapu? Na kumbuka waliotoka misri ni wawili tu na wengine walizaliwa tu njiani hatimae wakafika maelfu ya watu ...na bado haitoshi wakaangamia wote na wakabaki 2 tu waliongia kaanani yaani Joshua na Kalebu..1 Wakorintho 10:5
Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
👂Wapo watakao batizwa na kula pasaka kila mara lkn wasiingie mbinguni....Kati ya watu ambao aliwaona mama ellen G white wale watu 20 anasema aliowaona wakienda mbinguni hata hao 20 ni kwa shida sana kuwapata.
👂Tunaomba na tunasoma neno...lkn shida tulionayo hatupati md wa kutulia mara tunapomaliza kusoma neno au kusali. Maana Roho Mtakatifu hana mda na watu wenye haraka ili wawahi kwenye shughuli zao. Usiombe kisa una haraka kama unataka kupaa, pata mda wa kutafakari kile ulichokisoma .
👂Mwadventista msabato hacha kujifanya kuwa watoto ulionao ni wasabato halisi laaah! Wengine ni wapagani kabisa waombeee sana. Wewe mzazi hutakuwa na uwezo wa kuwaokoa watoto wao.
👂Nakuombea unapobatizwa na kula pasaka jitahidi kumaliza mwendo wako na usiwe kama wana Israel walioishia njiani.
👂Unapopatwa na matatizo katika safari yako ya Ukristo hakikisha unajitahidi kumaliza mwendo....Yesu atakupa taji ya uzima na atafurahi kukupokea.
Imeandaliwa vizuri na Mugeta Tz ....Admin wa Morning star radio fans 🌟
Barikiwa sana.....
Post a Comment