MAJALIWA AWATAKA MA RC KUTUNZA SIRI ZA SERIKALI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti utunzaji wa siri za Serikali katika maeneo wanayofanyia kazi

Akifungua Mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala na Mikoa Jana Jijini Dodoma Mhe Majaliwa amesema kuwa kuna wimbi limeibuka kwa baadhi ya barua kukutwa kwenye mitandao ya kijamii huku zikiwa na siri za Serikali hivyo Viongozi hao wanawajibu wa kuhakikisha siri za serikali hazisambai hovyo kwenye mitandao ya Kijamii

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia kwa barua za Serikali kuonekana kwenye mitanndao ya kijamii ikiwemo Whatsaap, Istragramm, twitter jambo hili ni aibu na sio usiri wa nyaraka za Serikali, hakikisheni mnalinda na kudhibiti utandawazi uliopo katika suala la utunzaji wa siri za Serikali.

Ameawataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia watumishi wa umma hasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili waweze kutunza siri za ofisi na kuwaelekeza kutumia mfumo unaokubalika katika utoaji wa taarifa na usambazaji wa nyaraka za Serikali

Wakati huohuo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema wataleta mapendekezo ya kuwapima wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri wote nchini kwa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi.
Ameendelea kusema kuwa Serikali inaenda kuchambua fedha inayobaki ya asimia 40 ya mapato ya ndani ili kuleta ulinganifu katika matumizi kulingana na umbali wa Halmashauri husika kwa kuwa serikali inataka fedha yote inayokusanywa kwenda kwenye miradi ya maendeleo.

“Kuna haja ya kuzichambua kwa kina matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali ambapo Halmashauri inayopata shilingi bilioni 1 kwa mwaka anaendesha Halmashauri kwa shilingi milioni 600 kwa mwaka na Halmashauri inayopata bilioni 5 kwa mwaka anaendesha Halmashauri kwa bilioni 2 na Halmashauri inayopata bilioni 20 wanaendesha Halmashauri kwa shilingi bilioni 8 kwa mwaka ambapo wakuu wa Idara ni haoahao

No comments