MHE. PAULINE GEKUL ATOA RAI KWA TFF
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul ametoa rai kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kutoa elimu kuhusu mawakala wa michezo na kwa siku za usoni itengeneze kanuni zitakazowasimamia mawakala hao.
Mhe.Gekul ametoa rai hiyo Julai 30 alipofungua Kongamano la wadau wa mpira wa miguu (Tanzania Football Summit 2021) linalofanyika kwa siku mbili Jijini Da er Salaam ambapo amesema ni vizuri wachezaji wote na vilabu kutumia mawakala pale wanaposajili wachezaji.
"Tanzania mpaka karne hii tuna mawakala takribani 6 tu nchi nzima ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ikiwemo AFRISOCCER Kampuni iliyoandaa kongamano hili, Idadi hii ni ndogo sana hairidhishi na hii inamaanisha wachezaji na wadau wa soka bado hawajafahamu umuhimu wa kutumia mawakala katika soka" amesema Mhe.Gekul
Naibu Waziri Gekul ameongeza kuwa Dunia ya sasa inakwenda kidijitali wachezaji wanauzwa na kutafutiwa timu kwa kutumia tovuti (Websites) na mifumo mbalimbali, pia taarifa za vilabu, wachezaji, makocha na mawakala katika ulimwengu wa sasa zinahifadhiwa kidijitali, Wachezaji wa kisasa wanafuata ratiba za mazoezi, aina za mazoezi na vyakula kidijitali. Hivyo ni wakati sasa nchi yetu kukimbizana na ulimwengu wa teknolojia hiyo.

Post a Comment