Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akinywa maji yanayozalishwa kupitia mtambo wa majisafi na Salama Ruvu Juu wakati wa ziara ya kukagua maboresho yaliyofanywa na DAWASA kwenye mtambo huo.
Aidha, Mhandisi @maryprisca_mahundi (Mb) amepata maelezo toka kwa Meneja wa @dawasatz Mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu, Mhandisi Edward Mkilanya kuhusu namna mtambo wa Ruvu Juu na maboresho yaliyofanywa kuongeza kiwango cha uzalishaji maji kufikia lita milioni 196 kwa siku.
Naibu Waziri yuko Jijini Dar es salaam kwenye ziara ya kutembelea miradi ya majisafi na usafi wa mazingira inayotekelezwa na @dawasatz.
0 Comments