Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 20

*JUMANNE, JULAI 20, 2021*

*KESHA LA ASUBUHI (KISWAHILI & ENGLISH), LESONI NA USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO*

```KESHA LA ASUBUHI

Jumanne, Julai 20, 2021

SOMO: KULA KWA AJILI YA NGUVU

 Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi. Mhubiri 10:17```

*Sheria za afya zinapaswa kutiiwa. Ni muhimu kwamba viungo vya mmeng'enyo visichoshwe. Kuna wengi ambao huweka tumbo kazini kila wakati. Halina nafasi ya kukusanya upya nguvu zake, na matokeo lazima yawe ni magonjwa yanayotokana na mmeng'enyo wa chakula*

Kusiwepo kula kati ya milo, na angalau saa tano zipite kati ya milo. Kuvimbiwa ni matokeo ya chakula kilichochukuliwa ndani ya tumbo kabla ya viungo vya mmeng'enyo kupata muda wa kuondoa mlo uliotangulia

*Milo mitatu inatosheleza, na milo miwili ni bora kuliko mitatu. Kwa miaka thelathini iliyopita nimekuwa nikila milo miwili tu kwa siku. Ugoigoi/uzito wa akili ambao unawasumbua watu mara nyingi husababishwa na kula kupita kiasi, na kwa kula katika vipindi visivyo rasmi-visivyofuata utaratibu. Kutomeng'enya chakula tumboni -kiungulia huleta hali ya kukata tamaa, na mtu anayesumbuliwa na ugonjwa huu, ingawa anaweza kudai kuwa Mkristo, anatenda kwa jinsi isiyo ya Kristo.*

Wengine wanadai kuwa kupenda kula ni kiashirio kinachotosheleza. Lakini mtu anaweza kuingia katika tabia ya kula mara kadhaa kwa siku, na hili si jambo bora kiafya. Tabia kama hiyo itasababisha magonjwa, kwa sababu viungo vya mmeng'enyo wa chakula vingelemewa

*Fanya matengenezo ya afya, na ukatae kupotoshwa kando ya njia sahihi. Usichoke, bali fanya utashi wako kuleta hamu yako ya chakula kuwa chini ya utawala wa kusudi la kweli....*

```Mungu alimpa Adamu usimamizi wa bustani ya Edeni, ailime na kuitunza, na katika miti na mimea inayozaa mbegu, Alisema, "Vitakuwa ndivyo chakula chenu" (angalia Mwanzo 1:29; 3:18). Baadaye ulaji wa nyama uliruhusiwa kama moja ya matokeo ya anguko. Kabla ya gharika, hakuna mtajo uliotolewa kwa ajili ya matumizi ya chakula kinachotokana na wanyama....

Jaribu kuishi bila kula nyama kwa miezi sita, na uone kama badiliko kuelekea ubora halitatokea. Ninakuomba ufanye hivi mara moja. Hebu fikra zako na zitakaswe. Hebu akili yako na dhamiri ziamshwe, utu wako wote utiwe nguvu. Jilinde dhidi ya kujihurumia sana. Kuwa shujaa. Dhamiria kushinda hamu potofu ya chakula.```

*MORNING DEVOTION*

TUESDAY, 20/07/2021

EAT FOR STRENGTH



*💪Blessed art thou, O land, when thy king is the son of nobles, and thy princes eat in due season, for strength, and not for drunkenness! Ecclesiastes 10:17.*

```✍🏿The laws of health are to be obeyed. It is important that the digestive organs shall not be overtaxed. There are many who keep the stomach continually at work. It has not opportunity to recruit its strength, and the result must be digestive disorders. 

✍🏿There should be no eating between meals, and at least five hours should be allowed to elapse between the meals. Indigestion is the result of food taken into the stomach before the digestive organs have had time to dispose of the foregoing meal.... 

✍🏿Three meals are sufficient, and two meals are better than three. For the past thirty years I have eaten only two meals a day. The dullness from which people suffer is often caused by overeating, and by eating at irregular periods. Dyspepsia brings despondency, and one suffering from this disease, though he may profess to be a Christian, acts in an un-Christlike manner. 

✍🏿Some claim that the inclination to eat is sufficient guide. But one may get into the habit of eating several times a day, yet this would not be best. Such a habit would produce disease, because the digestive organs would be overtaxed. 

✍🏿Practice health reform, and refuse to be turned aside from the right path. Do not faint away, but make your will power bring your appetite into subjection to a true purpose....

✍🏿God gave Adam charge of the garden of Eden, to dress it and to keep it, and of the trees and herbs bearing seed, He said, “They shall be for meat” (see Genesis 1:29; 3:18). Afterward the eating of flesh meat was permitted as one of the consequences of the fall. Before the flood, no provision was made for the use of animal food....``` 

*Try going without flesh meat for six months, and see if a change for the better does not take place. I ask you to do this at once.* 

*✍🏿Let your imagination be sanctified. Let your mind and conscience be awakened, your whole being aroused. Guard yourself against giving yourself too much sympathy. Be heroic. Be determined to overcome perverted appetite*.🔝
 

```LESONI, JULAI 20

SOMO: IMESAMEHEWA NA KUSAHAULIWA?

¶¶Baada ya Daudi kujitangazia hukumu juu yake mwenyewe (2 Sam. 12:5, 6), Nathani anamkabili kwa ukubwa wa ubaya wa dhambi yake. Moyo wa Daudi unavunjika, na anatubu dhambi yake. Mara moja Nathani anamhakikishia kwamba “ ‘BWANA naye ameiondoa dhambi yako’ ” (2 Sam. 12:13) na kwamba amesamehewa. Hakuna muda wa kusubiri kwa msamaha wa Mungu. Daudi hahitaji kuthibitisha kwamba ametubu kwa dhati kabla hajapatiwa msamaha. 

¶Hata hivyo, Nathani, ambaye amekwisha tabiri matokeo ya dhambi ya Daudi katika 2 Samweli 1: 10—12, anaendelea na kusema kwamba mtoto atakayezaliwa atakufa. 

✍🏽Inamaanisha nini kusema kwamba Mungu ameiondoa dhambi ya Daudi? Je, alisahau tu makosa yaliyopita na kuanza upya? Je, kila mtu hulisahau hilo kwa urahisi tu? Soma 2 Samweli 12:10—23 unapoyatafakari maswali haya.

✍🏽Lazima pia Daudi alishangaa kuhusu maswali haya alipoona mambo yakifaranghanyika—mtoto amekufa, familia yake iko kwenye machafuko (visa vya Amnoni na Absalomu ni mifano miwili mizuri ya matatizo halisi ya maisha ya familia), maisha yake yajayo yako gizani. Na licha ya matokeo ya dhambi yake, iliyowaathiri watu wasio na hatia kama vile Uria na mtoto aliyezaliwa, Daudi anaanza kuelewa kwamba neema ya Mungu itafunika hili na kwamba wakati unakuja matokeo ya dhambi yatatoweshwa. Wakati huo huo, anaweza kupata pumziko kwa ajili ya dhamiri yake iliyotaabika katika neema ya Mungu. 

¶Daudi anahisi kuhitaji nini hasa? Ana shauku ya kitu gani? Soma Zaburi 51:1—6.

¶¶Kwa Zaburi 51, Daudi anatoka hadharani akiufungua moyo wake na kutubu dhambi zake. Kilio cha Daudi kwa ajili ya rehema kinasihi upendo wa Mungu usioshindwa na huruma yake kuu. Ana shauku kwa ajili ya kufanywa upya. 

¶¶¶Tunapozingatia gharama ya pumziko ndani ya Yesu, tunahitaji kwanza kutambua kwamba tunahitaji msaada kutoka nje; sisi tu wenye dhambi tunamhitaji mwokozi; tunatambua dhambi zetu na kumlilia Yeye pekee awezaye kutuosha, kutusafisha, na kutufanya upya. Tunapofanya hili, tunaweza kuwa na ujasiri: huyu ni mzinzi, mdanganyifu, muuaji, na mtu aliyevunja angalau tano kati ya Amri Kumi anayehitaji msaada na kudai ahadi ya msamaha wa Mungu.

¶¶¶¶Ikiwa Mungu alimsamehe Daudi kwa kile alichokifanya, kuna tumaini gani, basi, kwa ajili yako?

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

YOHANA 14


1. Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 

2. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 

3. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 

4. Nami niendako mwaijua njia. 

5. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 

6. Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 

7. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 

8. Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 

9. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 

10. Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 

11. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 

12. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 

13. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 

14. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. 

15. Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 

16. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 

17. ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 

18. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 

19. Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 

20. Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 

21. Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 

22. Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 

23. Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 

24. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. 

25. Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 

26. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 

27. Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 

28. Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 

29. Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini. 

30. Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 

31. Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

MUNGU AKUBARIKI SANA```

Post a Comment

0 Comments