Advertisement

Responsive Advertisement

POLEPOLE AWANOA VIJANA, CHANGAMOTO ZA AJIRA

Mbunge wa kuteuliwa na Rais Humphrey Polepole amewaasa vijana wasichukulie fursa ya kilimo kama ushamba kwani Kwa sasa ajira ndio zimejikita huko. 

Polepole amewataka vijana hao kuunda vikundi na kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia kumi zinazotolewa na Halmashauri zote nchini. 

Sambamba na hapo pia amewataka vijana hao kutumia vyema mitandao ya kijamii kwa kutuma maudhui mazuri ambayo yatawawezesha kupata matangazo mbalimbali toka Kampuni binafsi na Serikali kwa ujumla. 

Polepole amekutana na kuzungumza na vijana hao katika Chuo cha Arusha University ambapo walihudhuria viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Arusha (UWT) Bi.Yasin Bach

Post a Comment

0 Comments