MFUMO WA TAARIFA ZA BIASHARA (TRADE PORTAL) WAZINDULIWA

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omari Said Shaaban pamoja na Naibu Waziri wizara ya viwanda na biashara Mhe. Exaud Kigahe wamezindua rasmi mfumo wa taarifa za Biashara (Trade Portal) utakaosimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Mhe. Omari Shaaban amesema kuwa "Taasisi za Umma na Sekta Binafsi zinapofanya mabadiliko ya taratibu zinazohusiana na taratibu za ufanyaji biashara ikiwemo utoaji wa vibali na leseni za kusafirisha bidhaa nje ya nchi, kuitaarifu TanTrade mapema ili iboreshe taarifa husika kwenye mfumo.” Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omari Said Shaban.

Naibu Waziri wizara ya viwanda na biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema kuwa "Utekelezaji wake ulianza rasmi tarehe 1 Julai 2017. Ambapo Wizara yetu iliupokea na kuuunganisha na Mfumo mkubwa wa utoaji wa Taarifa na Huduma za Biashara nchini (Tanzania National Business Portal) uliokuwa unatekelezwa pale Wizarani na baadae ulihamishiwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Utekelezaji wa Mfumo huu uliendelea kusimamiwa na BRELA mpaka pale Baraza la Uwezeshaji Biashara nchini lilipoamua kuuhamishia katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwani ndiyo yenye jukumu kisheria la kusimamia na kutoa Taarifa za Biashara nchini.”

Mradi huu wa mfumo wa taarifa za Biashara umefadhiliwa na wabia wa Maendeleo ambao ni Trade Mark East Africa (TMEA), ITC na MUARKUP Tanzania

No comments