MABULA AANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amenza kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero za ardhi katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Akiwa mkoani Morogoro katika ziara yake hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Dumila wilayani Kilosa walimueleza kuwa maeneo yao yana migogoro mingi ya ardhi jambo walilolieleza linalosababisha kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali.
Dkt Mabula alianza utekelezaji maagizo hayo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kikao cha ndani na viongozi wa wilaya ya Kilosa wakiwemo wenyeviti wa vijiji, watendaji wa mitaa, madiwani pamoja na wananchi waliowasilisha malalamiko kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Wakati wa kikao hicho, wenyeviti wa mitaa wakiongozwa na madiwani walieleza migogoro ya ardhi katika maeneo yao kuwa ni ile ya mipaka kati ya vijiji, kubomolewa kwa baadhi ya nyumba za wananchi, kutopimwa baadhi ya vijiji, wananchi kuzuiwa kuendelea na shughuli za kiuchumi na wanaodaiwa wamiliki halali pamoja na mgogoro ya uvamizi wa maeneo.
Akizungumza na viongozi hao tarehe 12 Julai 2021 wilayani Kilosa, Dkt Mabula alieleza kuwa, migogoro mingi ya ardhi imesababishwa na wenyeviti wa vijiji hasa katika suala la ugawaji ardhi na kusisitiza kuwa mwenye mamlaka ya kugawa ardhi ya kijiji ni mkutano wa kijiji na siyo mwenyekiti wa kijiji na ardhi hiyo haitakiwi kuzidi ekari 50.
" Kasimamieni vizuri vijiji vyenu na mhakikishe ardhi katika maeneo yenu inapimwa na kupangwa maana itapunguza migogoro ya ardhi katika maeneo yenu" alisema Dkt Mabula.

Post a Comment