LUKUVI AONYA UMILIKISHAJI VIWANJA MARA MBILI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema watumishi wa sekta ya ardhi watakaohusika kwa namna moja ama nyingine kumilikisha kiwanja kimoja mara mbili (Double allocation) watachukuliwa hatua kali.
 
Alizungumza mara baada ya kukagua shughuli za utendaji wa sekta ya ardhi kwenye Banda la Wizara ya Ardhi katika maonesho ya 45 Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba alisema, ikibainika kuna umilikishaji mara mbili uliosababishwa na watumishi basi wote waliohusika kama ni afisa upimaji, upangaji na mmililishaji wote watachukuliwa hatua.

Alisema, awali sekta ya ardhi ilikuwa na migogoro mingi lakini tangu mwaka 2015 kero nyingi za sekta hiyo hazipo ama zimepungua kwa kiasi kikubwa.
 
" Ni kweli huko nyuma tulikuwa na kero nyingi sana katika sekta ya ardhi na ninaamini tangu mwaka 2015 migogoro hakuna ama imepungua sana na nisisitize kama kuna utoaji hati mara mbili wote walioshiriki kuanzia wale wa kupima, kupanga na yule aliyemilikisha watachukuliwa hatua" alisema Lukuvi.

No comments