CHANJO KUANZA KUTOLEWA AGOSTI 3 KATIKA MIKOA YOTE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema Chanjo itaanza kutolewa 3 Agosti 2021 katika Mikoa yote, vituo 550, viituo vitaongezwa katika Wilaya na Halmashauri.

Aidha, ametaja mambo ya kuzingatia kabla ya kuchanjwa kwanza, kujitathmini kama upo kwenye makundi ya walengwa, kuandaa kitambulisho cha kazi, NIDA, Leseni ya udereva, Mpiga kura, pasi ya kusafiria au kitambulisho chochote kinachotambulika kisheria, kufanya booking ya siku ya kuchanjwa kwa kutumia mtandao ndani ya simu au kompyuta (Online) kupitia www.chanjocovid.moh.go.tz au kwenda moja kwa moja kwenye kituo na kujisajili kuanzia Jumatatu tarehe 2/8/2021, kujaza fomu ya uhiari wa kuchanjwa.

"----->Chanjo hizi kwa sasa zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa ambayo ni:,Watumishi wa sekta ya afya (umma na binafsi), watu wazima umri wa miaka 50 na kuendelea, mtu mwenye magonjwa sugu na ya muda mrefu"---- MAKUBI

Katika Makundi mengine ya wananchi amesisitiza yatapata chanjo katika awamu inayofuata.

No comments