CHADEMA WAPANGA AGOSTI 5 IWE NI SIKU YA KUPINGA UONEVU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia katibu mkuu, Mhe. John mnyika wametangaza siku ya Alhamisi, 05 August 2021, iwe ni siku ambayo ni maalum ya kupinga uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi ambao unafanywa kwa Mhe. Freeman Mbowe nchi nzima, "Hii nisiku ambayo FREEMAN MBOWE atapandishwa mahakamani"---- JOHN MNYIKA
Aidha, amesema baaada ya kujidhihirisha kutoka vyanzo mbalimbali wamefanikiwa kupata utajiri wa taarifa na hivyo wanasema kwamba, mashtaka yanayomkabili Freeman Mbowe ni ya kupika na hivyo kuna haki ya kujadili nje ya mahakama ili kumtaka DPP aondoe shtaka hilo na Mwenyekiti wao atoke.
"Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi mfululizo kujadili masuala yanayohusu chama hiko ikiwemo sakata la kukamatwa na kushtakiwa Mwenyeki wao Freeman Mbowe, kwa kauli moja imeazimia kufungua kesi ya kikatiba kupinga ukiukwaji wa katiba na sheria katika sakata linalomuhusu Mbowe"---- JOHN MNYIKA
"Kamati Kuu ya Chadema imepitiabna kujiridhisha hati ya mashtaka na mashtaka aliyotuhumiwa nayo Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, na kubaini kuwa, hati hiyo ya mashktaka imekosa mashiko na uhalali wa kisheria na huenda imetumika kama mbinu ya kummaliza kisiasa" ---- JOHN MNYIKA
Post a Comment