CCM KUIMARISHA ZAIDI VYOMBO VYAKE VYA HABARI

Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka, amefanya ziara ya kawaida *Jumamosi 03 Julai 2021* katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi.

Akitoa salaam za CCM kwa watumishi wa vyombo hivyo amesema mkakati uliopo sasa ni kuviimarisha vyombo vyote vya habari vya Chama pamoja na kushughulikia kwa haraka changamoto mbalimbali zinazokwamisha ufanisi wa kazi katika vyombo hivyo.

Shaka amefahamisha kuwa lengo na dhamira ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha vyombo vya habari vya CCM vinaimarika zaidi na kufikia malengo yake katika kuhabarisha umma kuhusu mambo mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.

Vyombo vya habari vya CCM ni pamoja Channel Ten, Channel Ten Plus, Magic Fm, Classic FM, Uhuru Fm, Gazeti la Uhuru na Mzalendo.

No comments