AZAM FC WAMSAJIRI IDRIS MBOMBO KUTOKEA CONGO

Klabu ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo, aliyemunuliwa kutoka El Gouna (@gounafc) ya Misri.

Mbombo amesaini mkataba huo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kuhudumu ndani ya timu hiyo hadi mwaka 2023.

Mshambuliaji huyo hatari, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors (zote za Zambia), ametajwa kuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji klabuni hapo.

Huo unakuwa usajili wa sita kwa Azam FC, kwenye dirisha hili wakijiandaa na msimu ujao.

"Awali tukiwasajili nyota watatu kutoka Zambia, Charles Zulu, Paul Katema, mshambuliaji Rodgers Kola, Mkenya Kenneth Muguna na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama."---- AZAM FC

No comments