ALIYEJARIBU KUMCHOMA KISU RAIS WA MPITO MALI, AFARIKI DUNIA

Mwanaume anayetuhumiwa kujaribu kumchoma kisu Rais wa mpito wa Mali, Assimi Goïta, wiki iliyopita amefariki dunia hospitalini akiwa chini ya ulinzi, serikali ya nchini humo imesema.

Mshambuliaji huyo, ambaye hajatambuliwa, alikamatwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio lake, ambalo lilifanyika wakati Bwana Goïta akihudhuria sala katika msikiti sikukuu ya Eid al Adha.

Taarifa ya serikali ilisema afya ya mtu huyo ilikuwa imezorota akiwa chini ya ulinzi na alipelekwa hospitalini, ambako alikufa, chanzo cha kifo chake bado kinachunguzwa.



No comments