Advertisement

Responsive Advertisement

WANACHAMA WA SADC NCHINI WAPITISHA MKAKATI MPYA

Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wanaohusika na Mazingira, Maliasili na Utalii, wamepitisha mkakati wa misitu wa miaka 10 kuanzia 2020 hadi 2030, kwa nchi wanachama unaolenga kukuza na kusimamia biashara ya rasilimali misitu.

Kikao cha mawaziri hao kilichoitishwa na sekretarieti ya SADC, kimejadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Itifaki ya SADC ya Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya kujenga maendeleo endelevu, mkakati wa SADC wa mabadiliko ya tabianchi na Mpango kazi wa utekelezaji wake

Pia kimejadili mkakati wa jumuiya wa kudhibiti ujangili na itifaki ya kuendeleza utalii katika nchi wanachama ambapo taarifa ya kikao hicho imetolewa na naibu Waziri wa maliasili na Utalii Mary Masanja baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao.

Kikao hicho kimekuwa kikifanyika kila baada ya miaka miwili ambapo mwaka 2019, kilifanyika hapa nchini wakati Tanzania ikiwa ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Post a Comment

0 Comments