UMMY MWALIMU ATEMBELEA UTEKELEZAJI MIRADI KAHAMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe Ummy Mwalimu tarehe 29/05/2021 ametembelea utekelezaji miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Miradi iliyoikagua ni ujenzi wa Kituo cha afya cha Nyasubi, eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda vidogo na wajasiriamali wadogo, shule ya sekondari ya Nyingo, ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama na jengo la utawala, miradi hii imetekelezwa kwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri


Aidha amewapongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya maendeleo.

No comments