TANZANIA KUENDELEA KUONGOZA BARANI AFRIKA

Tanzania imedhamiria kuendelea kuongoza barani Afrika kwa uzalishaji wa zao la pareto toka tani 3000 mwaka 2021 hadi kufikia malengo ya tani 9,000 kutokana na uwepo wa viwanda vitatu vya kuongeza thamani zao hilo.

Hayo yamebainishwa (28.05.2021) jijini Dodoma wakati wa kikao cha wadau wa zao la pareto toka mikoa sita nchini kilichoshirikisha viongozi wa mikoa, wilaya ,halmashauri, makampuni ya pareto na wawakilishi wa wakulima.

Akizungumza kwenye kikao hicho Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliwapongeza wadau kwa kuweka lengo hilo la kufikisha tani 9,000 za maua ya pareto ambapo viwanda vitatu vilivyopo sasa vitaweza kuinunua yote kulingana na uwezo wake.

Bashe alisema ili kufikia malengo hayo ya uzalishaji wizara kupitia Bodi ya Pareto na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) itawekeza kwenye utafiti wa mbegu bora za pareto na kuhakikisha zinapatikana kwa wingi na kugawiwa kwa wakulima nchini.

"Tunahitaji mbegu bora za pareto tani 3 ili zitumike kuzalisha tani 9,000 za pareto baada ya mwaka mmoja ambapo viwanda viko tayari kuinunua toka kwa wakulima alisisitiza Bashe

Naibu Waziri huyo alizipongeza Kampuni ya Pareto Tanzania (PCT) ambayo itanunua tani 6,000 kwa mwaka huku kampuni ya TAN Extract Ltd ikihitaji tani 1,000 na kampuni ya PYTECH Ltd ikihitaji tani 2,000 za maua ya pareto itakayozalishwa na wakulima msimu wa 2022/23.

Katika hatua nyingine Bashe alibainisha mikakati ya wizara kuhakikisha zao la pareto linakuwa na tija na uzalishaji wake unaongezeka zaidi ambapo alitaja mambo sita .

Kwanza kuongeza utafiti na uzalishaji wa mbegu bora tani 3 kupitia TARI, pili kuanzisha mfumo wa kilimo mkataba (Contract Farming), tatu kuanzisha mfumo wa ushirika kwa kuanzisha AMCOS za wakulima wa pareto.

No comments